Austria
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: “'Land der Berge, Land am Strome“ (Kijerumani kwa "Nchi ya milima, nchi ya mtoni") |
|||||
Mji mkuu | Vienna |
||||
Mji mkubwa nchini | Vienna | ||||
Lugha rasmi | Kijerumani 1 | ||||
Serikali
Rais
Chansella |
Jamhuri Heinz Fischer Alfred Gusenbauer |
||||
Uhuru Mkataba kuhusu Austria ulianza Tangazo la baki |
27 Julai 1955 26 Oktoba 1955 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
83,871 km² (ya 115) 1.3 |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
8,292,322 (ya 9) 8,032,926 99/km² (ya 99) |
||||
Fedha | Euro (€) 2 (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .at 3 | ||||
Kodi ya simu | +43 (details) |
||||
1 Kislovenia, Kikroatia, Kihungaria ni lugha rasmi kieneo. 2 Kabla ya 1999: Shilingi ya Austria. |
Austria (Kijer.: Österreich) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Uceki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi Liechtenstein. Mji mkuu ni Vienna.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Eneo la nchi lina umbo ndefu na nyembamba kama kanda linaloelekea kutoka mashariki kwenda magharibi. Sehemu kubwa ya Austria (60%) ni milima. Tambarare ziko hasa kando la mto Danubi ambao ni pia mto mkubwa. Theluthi moja la eneo liko chini ya 500 m. Zaidi ya 40% za nchi ni misitu. Mto Danubi unavuka sehemu kubwa ya nchi.
Milima mikubwa ya Austria inafikia kimo kati ya 3000 na 4000 m. Katika hali ya hewa ya nchi kuna theluji mwaka wote. Mlima mkubwa ni Grossglockner mwenye 3,798 m halafu Wildspitze mwenye 3,774 m juu ya UB.
Ziwa kubwa ni ziwa la Neusiedler See lililopo mpakani na Hungaria. Mlimani kuna maziwa mengi madogo. Uso huo wa nchi ni msingi wa utalii ulio muhimu sana Austria. Wakati wa joto watalii wanaponda baridi ya milima; wakati wa baridi wanakuja kwa kucheza ski.
[hariri] Utamaduni na lugha
Watu wa Austria huzungumza Kijerumani ambacho ni pia lugha rasmi. Mpakanai upande wa kusini na mashariki kuna pia wasemaji wa Kikroatia, Kislovenia na Kihungaria. Lugha hizi zina cheo rasmi kieneo au kitarafa.
Kwa jumla lahaja na utamaduni hufanana katika mengi ile ya Wabavaria katika jimbo la jirani la Ujerumani.
[hariri] Miji
- Wien (Vienna)
- Graz
- Linz
- Salzburg
- Innsbruck
[hariri] Historia
Austria kama nchi ndogo jinsi ilivyo imepatikana tangu 1918 mwishowe tangu 1945. Kwa muda mrefu wa historia yake Austria ilihesabiwa kama sehemu ya Ujerumani. Kwa karne nyingi watawala wake walishika cheo cha Kaisari wa Dola takatifu la Roma lililojumlisha Ujerumani wote. Austria ilitawala pia sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki.
Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari Franz II alilazimishwa kujiuzulu kama Kaisari la Ujerumani wote mwaka 1806 akabaki na cheo cha Kaisari wa Austria tu. Baada ya Napoleoni Austria ilikuwa nchimuhimu katika shirikisho la Ujerumani. Mwaka 1866 Austria ilishindwa katika vita dhidi Prussia ikatoka katika siasa ya Ujerumani.
Hadi Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia Austria iliendelea kutawala nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na Uceki, Slovakia, Slovenia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina, Hungaria na sehemu kubwa ya Poland ya Kusini, pia sehemu zilizopo sasa chini ya Italia. Mwisho wa vita dola hili liliachana na nchi ndogo iliyokaliwa na Waaustria Wajerumani ilibaki. Washindi wa vita vilizuia Waaustria wasijiunge na Ujerumani hivyo Jamhuri ya Austria ilianzishwa.
Mwaka 1938 dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler (aliyekuwa Mwaustria mwenyewe) alivamia Austria kwa jeshi lake na kuiunganisha na Ujerumani. Wakati ule sehemu kubwa ya Waaustria walikubali.
Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Austria ilirudishwa kama nchi ya pekee ikabaki hivyo.
1995 Austria ikajiunga na Umoja wa Ulaya.
[hariri] Waaustria Mashuhuri duniani
Wolfgang Amadeus Mozart Sigmund Freud Adolf Hitler Arnold Schwarzenegger Kurt Waldheim
Nchi na maeneo ya Ulaya | |||
---|---|---|---|
Albania | Andorra | Austria | Belarus | Bosnia na Herzegovina | Bulgaria | Kroatia | Denmark | Eire | Estonia | Ufaransa | Hungaria | Iceland | Italia | Jamhuri ya Masedonia | Latvia | Liechtenstein | Lithuania | Luxemburg | Malta | Moldova | Monako |Montenegro | Norway | Poland | Romania | San Marino | Serbia3 | Slovakia | Slovenia | Hispania | Ubelgiji | Uceki | Ufini | Ugiriki | Ujerumani | Uholanzi | Ureno | Urusi1 | Uswidi | Uswisi | Ukraine | Uingereza | Vatikani
Maeneo ya Ulaya ya kujitawala chini ya nchi nyingine: Visiwa vya Faroe | Gibraltar | Guernsey | Jan Mayen | Jersey | Isle of Man | Svalbard Nchi za Asia ambazo ni mwanachama wa baraza la Ulaya au vyombo vingine vya Ulaya: Armenia2 | Azerbaijan1 || Cyprus2 | Georgia1 | Kazakhstan1 | Uturuki1 Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa: Abkhazia | Nagorno-Karabakh2 | Ossetia ya Kusini | Transnistria | Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini2 Maelezo: (1) nchi ya kimabara katika Asia na Ulaya; (2) nchi katika eneo la Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) lakini kiutamaduni huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya; (3) Inaelekea kugawiwa kuwa nchi mbili za Serbia na Montenegro
|