Arnold Schwarzenegger
Kutoka Wikipedia
Arnold Schwarzenegger (amezaliwa tar. 30 Julai, 1947 nchini Austria) ni mwigizaji wa filamu na ni Gavana wa sasa wa jimbo la Californiaa nchini Marekani. Arnold anaishi mjini Los Angeles, California, lakini anafanya kazi huko Sacramento, ambapo ni mji mkuu wa jimbo la California.
Schwarzenegger alielekea nchi Marekani mnamo mwaka wa 1968 na kisha baadaye akawa mwigizaji wa filamu. Ameigiza filamu nyingi tu, ikiwemo ile ya The Terminator na nyingine nyingi tu. Mnamo mwaka wa 2003, pale Bw. Gray Davis alipoondoka madarakani, Schwarzenegger akashinda kiti cha kuwa Gavana wa California.
Schwarzenegger ameoana na Bi. Maria Shriver.
Kabla ya kuwa mwigizaji, kwanza alikuwa Mnyanyua Vyuma. Kwa kigezo hicho akafanikiwa kuwa Bw. wa ulimwengu kwa takriban mara saba.
[hariri] Viungo vya nje
- Arnold Schwarzenegger katika Internet Movie Database
- Arnold Schwarzenegger Bodybuilding Gallery (Gallery of Arnold Schwarzenegger's Competitive Years)