•Makala maalum:
Barack Hussein Obama (* 4 Agosti 1961) ni mwanasiasa nchini Marekani na tangu 2004 yeye ni seneta wa jimbo la Illinois katika bunge la kitaifa. Tangu mwaka 2007 ametafuta nafasi ya mgombea wa chama cha Demokrasia (Democratic Party) kwa uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008.
Alipoingia bungeni alikuwa seneta wa kitaifa wa pekee Mwamerika mweusi
Utoto na Ujana
Baba yake Obama alikuwa Mkenya Barack Obama aliyeaga dunia 1982. Mzee Obama alitoka mkoa wa Nyanza nchini Kenya akaenda Marekani masomoni. Mama alikuwa Mwamerika mzungu Ann Dunham kutoka jimbo la Kansas aliyeaga dunia 1995. Wazazi walifunga ndoa wakati ndoa kati ya watu weupe na weusi bado ilikuwa marufuku katika sehemu za kusini za Marekani. Wazazi waliachana baada ya miaka miwili na mtoto Barack alibaki na mama.
Mama aliendelea kuolewa na mwanafunzi kutoka Indonesia akamfuata aliporudi kwake. Hivyo Barack aliishi Jakarta hadi 1971 aliporudi Marekani na kukaa na babu yake huko Hawaii hadi alipomaliza shule ya sekondari.
Barack ana dada wawili mmoja kutoka ndoa ya pili ya mamake na mmoja kutoka ndoa wa pili wa babake huko Kenya.
•Ujenzi
Ujenzi - Usanifu -
•Usanii
Fasihi - Ushairi - Bombwe - Ngoma - Uchoraji-
Kiswahili - Sheng - Lugha za Kibantu - Kiingereza - Lugha za Kirumi - Kiesperanto -
Mmomonyoko - Afrika - Shaka Zulu - Mapigano ya Adowa - Reli ya Uganda - Madola -
Akiolojia - Falaki - Biolojia - Kemia - Fizikia - Tiba - Elimu - Lugha - Hisabati - Sayansi - Teknolojia
•Jumuiya
Sheria - Siasa - Dini - Utabiri wa nyota
|