Mapigano ya Adowa
Kutoka Wikipedia
Mapigano ya Adowa yalitokea 1 Machi 1896 katika nyanda za juu za Tigray kati ya jeshi la Italia kwa upande mmoja na la Ethiopia kwa upande mwingine. Ushindi wa Ethiopia ulihakikisha uhuru wa nchi.
Yaliyomo |
[hariri] Utangulizi
Mwaka 1889 mtemi wa Shewa Menelik II alijitangaza Negus wa Ethiopia baada ya kushinda mapigano kazi ya watemi wa Ethiopia yaliyofuata kifo cha Negus aliyetangulia Yohanne IV. Menelik alisaidiwa na Waitalia walioshika tayari Eritrea. " Mei 1889 Menelik alifanya mkataba wa Wuchale alimokubali utawala wa Italia juu ya kanda ya pwani pamoja na maeneo kadhaa ya nyanda za juu za Tigray yakiwemo mazingira ya Asmara ya leo.
Italia ilidai kutokana na nakala ya Kiitalia ya mkataba huo haki ya ulinzi juu ya Ethiopia. Menelik aliiimarisha utawala wake na mwaka 1893 alikana mkataba.
[hariri] Italia inavamia Ethiopia
Italia ilijibu kwa kuvamia Ethiopia kwa jeshi kubwa katika Oktoba 1895. Menelik aliweza kukusanya takriban wanajeshi 100,000 na kuwaongoza Tigray (jimbo jirani ya Eritrea).
Mapigano ya kwanza ndani ya Tigray ya Amba Alagi (7 Desemba) na ya Mekelle hayakuenda vizuri kwa Waitalia. Waethiopia walishindwa kuteka boma la Mekelle lakini Waitalia walifungwa ndani kwa wiki tatu. Mwishowe waliondoka baada ya mapatano na Negus Menelik II na kurudi Eritrea.
Sehemu kubwa ya jeshi la Italia haikuingia bado katika mapigano. Gavana jenerali Oreste Baratieri alikataa kuwashambulia Waethiopia baada ya kujua idadi yao kubwa. Alijua ya kwamba Menelik asingeweza kulisha askari wengi hivi kwa muda mrefu katika milima ya Tigray akataka kusibiri hadi jeshi la Negus lilianza kusikia njaa na kupungua.
Lakini serikali ya Roma ya waziri mkuu Francesco Crispi baada ya kupokea habari za mapigano ya kwanza iliona aibu ya kushindwa na Waafrika ikamwamuru gavana ashambulie mara moja.
[hariri] Adowa
Baratieri aliongoza jeshi lake la vikosi vinne katika milima ya Tigray.
Jeshi lake lilikuwa na vikosi vitatu vya Waitalia na kikosi kimoja cha askari kutoka Eritrea. Jumla ya wanajeshi ilikuwa 17,700 na mizinga 65. Hii ilikuwa nusu ya Waitalia wote waliopatikana katika Eritrea.
Baratieri alijua ya kwamba kulikuwako kambi kubwa ya Waethiopia karibu na mji wa Adowa alitaka kuwashambulia asubuhi wakati wa kucha kabla hawakuamka. Lakini vikosi vyake walipotea njia gizani waliposogea mbele usiku hawakufika kwa utaratiibu mzuri mahali walipokutana na jeshi la Negus.
Jeshi la Menelik lilikuwa la wanajeshi 80,000 hadi 100,000. Wengi wao walikuwa na bunduki zilizonunuliwa katika miaka iliyotangulia na Menelik kutoka wafanyabiashara Waitalia.
Wakati wa asubuhi wa 1 Machi 1886 kikosi cha kwanza cha askari Waeritrea chini ya maafisa Waitalia kiligonga moja kwa moja kambi la Ras Alula aliyekuwa tayari. Makelele yaliamsha Waethiopia wote waliochukua haraka nafasi zao juu ya milima wakiwashambulia Waitalia waliosogea mbele bondeni.
Baada ya masaa sita mapigano yalikwisha. Waitalia walishindwa, wengi kuuawa na wengine walikimbia wakirudi Eritrea. Wanajeshi wao 7,000 waliuawa na 1,500 kujeruhiwa, 3,000 wakawa wafungwa kati yao jenerali mmoja. Waethiopa walipoteza 4,000 - 5,000 na 8,000 kujeruhiwa. Waitalia walipaswa kuacha nyuma mizinga yote na bunduki 11,000 na vifaa vingi.
Menelik hakuwafuata Waitalia ndani ya Eritrea. Sababu hazieleweki wazi wazi lakini wataalamu hutaja sababu mbalimbali:
- Menelik alijua hata kama angewafukuzwa Waitalia wote katika Eritrea angejiweka katika hatari ya kupelekwa kwa jeshi lote la Italia dhidi yake kwa sababu Italia itajaribu kuondoa aibu. Alijua ya kwamba asingeweza kushinda vita kamili dhidi ya nchi iliyoendelea.
- Menelik alikuwa aliandaa kuvunja jeshi kabla ya mapigano lake kwa sababu vyakula vilikwisha katika Tigray kutokana naidadi kubwa ya wanajeshi kutoka nani ya nchi. Aliona ugumu jinsi gani kulisha idadi kubwa.
- Menelik alikumbuka mkataba wake wa kwanza alimokubali utawala wa Italia katika Eritrea.
[hariri] Baada ya mapigano
Waethiopia waliwatendea wafungwa Wazungu vizuri lakini walikata 800 askari wafungwa Waeritrea mkono na mguu wa kuume.
Baada ya habari hizi kufika Italia serikali ya Crispi ilipinduliwa. Serikali mpya ilipaswa kukubali uhuru wa Ethiopia katika mkataba wa amani 26 Oktoba 1896. Ethiopia ilikubali mamlaka ya Italia juu ya koloni yake katika kaskazini. Wafungwa walirudishwa.
Ushindi wa Menelik ulihakikisha uhuru wa Ethiopia kama nchi ya pekee pamoja na Liberia isiyowekwa chini ya ukoloni wa Ulaya katika bara la Afrika.