Sayansi
Kutoka Wikipedia
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli zilizo bainishwa pasi kuthibitishwa.
Yaliyomo |
[hariri] Aina Za Sayansi
Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika:
Sayansi Asili k.m.
Sayansi Umbile k.m.
Sayansi Jamii k.m.
- Arkiolojia
- Elimu
- Saikolojia
- Siasa
Sayansi Tumizi k.m.
Pia, kuna sayansi zinahusu mada mbalimbali:
[hariri] Metodi za Kisayansi
Msingi wa sayansi ni vitendo.
Vitendo vya Kisayansi vina njia zake zinazotumikia kusimamisha kweli ya kisayansi.
Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka Nadharia ama Udhanifu. Halafu tena ili Kweli ikubalike; hutoka kwenye udhanifu; kwa kupitia kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.
Kwa hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaumba nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Isipokuwa kweli watakanusha nadharia hii. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa ni nadharia inayokubalika.
[hariri] Sura ya Kisayansi
Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kuwa pingifu ya Hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika Jiwe (Maada Yabisi) kuna uvungu ( dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.
[hariri] Historia
[hariri] Sura ya Kiutamaduni
Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmoja mmoja; lakini kadri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wakujitenga. hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo ilionekana kama ni shauku la mtu mmoja mmoja kama awali.
Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa ni sehemu ya historia ya Sayansi. Majina na sifa kutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.
Sayansi na Jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.
[hariri] Sayansi Na Siasa Za dunia
Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.
Ingawaje haibanishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu kimamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.
[hariri] Sayansi Na Maendeleo
Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu kuwa mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.
Na hivyo roho ya uchunguzi ndio iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.
Makala hiyo kuhusu "Sayansi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sayansi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |