Fizikia
Kutoka Wikipedia
Fizikia (kutoka kigiriki φυσικός (physikos), "maumbile", na φύσις (physis), "kiumbo") ni sayansi inayohusu maumbile ya Dunia, ambayo inahusu asili ya viungo vya ulimwengu.
Ni taaluma kutoka shina la sayansi yenye kushughulika na Maada na uhusiano wake na Nishati.
Yaliyomo |
[hariri] Utangulizi
Tangu zama za nyuma kabisa, wanafalsafa ya asili walijaribu kueleza mafumbo kama vile mienendo ya sayari na asili ya maada. Na Mlengo huu ulijulikana hapo mwanzo kama Fizikisi(kut. eng., Physics, ikiandikwa Physike kuiga dhana ya Aristotle). Kuibuka kwa Fizikia kama tawi la sayansi lenye kujitegemea toka kwenye shina falsafa asilia, kulitokana na mapinduzi ya kisayansi ya karne ya 16 na 17 na kuendelea mpaka pambazuko la Sayansi ya Kisasa, mnamo mwanzo wa karne ya 20. Nyanja hii imekuwa ikiendelea kutanuka kulingana na kukua kwa tafiti na kupelekea gunduzi mbali mbali kama vile; modeli sahili ya chembe za kimsingi na uelezi uliotanuka wa historia ya ulimwengu, sambamba na mapinduzi ya tekinolojia mpya kama silaha za kinyuklia na semikonda. Leo hii Utafiti unaendelea katika mikondo mipana ya ki mada; kuhusisha mpitishoumemkuu katika joto la hali ya Juu, Ukototiaji wa Kikwantumu, utafutaji wa Higg Boson, na jitahada za kuendeleza Nadharia ya Mtuazi wa Kikwantumu. Uliokitwa katika Mitazamo na vitendo, na pia seti zilizojisheheneza kwa nadharia zinazodhihirishwa kwa Hisabati nzuri, Fizikia imefanya mchango mwingi katika sayansi, tekinolojia na falsafa.
Ugunduzi katika Sayansi umegusa kote ndani ya Sayansi Asilia, na Fizikia inaelezwa kama Sayansi ya Msingi kwa sababu nyanja zingine kama Kemia na Baiolojia, huchunguza mifumo ambayo tabia zake husimama toka kwenye kanuni za Fizikia. Kemia, kwa mfano, ni sayansi ya dutu iliyofanyika na atomu na molekyuli kwa wingi mmoja, lakini tabia za kampaundi za kikemia zinatathminiwa kwa tabia za kimaumbile za molekyuli zinazochipukia kwayo.
Fizikia ya vitendo inahusiana kwa karibu na Uhandisi na Tekinolojia. Mwanafizikia anayejihusisha na msingi wa utafiti hufanya muundopicha na kisha kufanya vitendo kwa kutumia vyombotekichi kama kikazanishio mwendo wa chembe na Biru, na angali mwanafizikia anayejihusisha na tafiti zilizotendewa kazi, huvumbua tekinolojia kama vile Upigaji Picha Kiusumaku Mtetemiazi (Kut. eng. MRI, Magnetic Resonance Imaging) na tranzista za sifa mbali mbali.
Fizikia ya kinadharia ina uhusiano wa karibu na hisabati, ambayo huipa lugha ya nadharia za kimaumbile. Aghalabu ni kweli kwamba shauri la kwanza la Nadharia ni kupembua mahusiano katika sura ya ki ulimwengu inayo shahibiana na yatendekayo, kazi ingine ya umuhimu sawa ni kufanyiza kanuni za mahusiano kimahesabu. Matumizi ya hisabati katika nadharia huwakilisha dhana ya kimawazo, katika mchakato wa kuibua mhitimisho muhimu kutoka kwenye hali ya Udhanifu uliopitia sheria rasmi za ukokotoaji. Hata hivyo, nafasi ya hisabati katika nyanja ya Fizikia ya Kinadharia inapelekea kwamba, si tatizo la mwanafizikia ya kinadharia ku chetua kidhibitihakikivu cha kihesabu na, kwa kweli kabisa; mahitaji yaliyokaza sana kwenye hesabu mara nyingi hupingana na kweli za kimaumbile. Mwanafizikia ya Kinadharia maranyingi vile vile huegamia katika ufuatiliaji tathmini wa kinamba na uchocheaji picha wa kompyuta na hivyo kuona matokeo yake; na ndio maana kompyuta na kuprogram kompyuta imekuwa na uwanda mpana wenye sura mbali mbali katika kufanya modeli za kimaumbile. Kwa kweli, nyanja ya Hisabati na Ufuatiliaji tathmini kikompyuta ni uwanja uliochangamka katika utafiti. Fizikia ya kinadharia mara nyingi huhusiana na falsafa na metafizikia ambapo inaangukia upande wa mawazo ya kufikirika kama vile Spesi za vizio wakadhaa na yunivesi sambamba.
[hariri] Nadharia
Ingawaje mwanafizikia husoma aina mbali mbali za mafumbo ya maisha, kuna baadhi ya nadharia zinatumika kwa wanafizikia wote. Kila moja ya hizi nadharia imejaribiwa kwa idadi ya vitendo na kuhakikishwa makadirio sahihi ya asili iliyopo ndani ya mizingo yenye kukubadilika umakini. Kwa mfano, nadharia ya