Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Akiolojia - Wikipedia

Akiolojia

Kutoka Wikipedia

Wanakiolojia wakichimba kwenye misingi ya maghofu ya monasteri huko Sweden
Wanakiolojia wakichimba kwenye misingi ya maghofu ya monasteri huko Sweden
Barabara hii ya Pompei (Italia) ilifunikwa mwaka 79 na majivu ya volkeno kwa muda wa miaka 1800 hadi kufunuliwa tena na wanakiolojia kuanzia 1863
Barabara hii ya Pompei (Italia) ilifunikwa mwaka 79 na majivu ya volkeno kwa muda wa miaka 1800 hadi kufunuliwa tena na wanakiolojia kuanzia 1863

Arkiolojia (kutoka Kiyunani αρχαίος = zamani na λόγος = neno, usemi) ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Waarkiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengo, makaburi, silaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu.

Tofauti na somo la Historia haichunguzi maandishi hasa ili kupata ufafanuzi juu ya mambo ya kale. Historia ikiangalia habari arkiolojia huangalia vitu. Waarkiolojia wanaweza kutumia maandishi na habari za historia wakiamua jinsi gani kuendelea na utafiti wao, kwa mfano wachimbe wapi. Lakini hutumia mitindo ya sayansi mbalimbali kuchunguza vitu vinavyopatikana kwa njia ya arkiolojia.

Mfano bora wa arkiolojia ni utafiti wa mji wa Pompei huko Italia. Habari za Pompei zimepatikana katika maandishi mbalimbali ya kiroma lakini mji uliharibika kabisa na kufunikwa na majivu ya volkeno Vesuvio mn. mwaka 79 b.K. Kuanzia mwaka 1748 wataalamu walianza kuchimba mahali pa mji mpotevu wakaipata. Hadi leo sehemu kubwa ya mji umefunuliwa tena. Chini ya majivu na udongo wa karne nyingi vitu vingi vimehifadhiwa vizuri ambavyo vingepotea kabisa visingefunikwa, kwa mfano picha za kiroma kwenye kuta za nyumba zenye rangi nzuri kabisa. Hata mabaki ya chakula yamepatikana yakachunguliwa.

Afrika na Arkiolojia: ujuzi wa arkiolojia ni muhimu sana kwa ajili ya historia ya Afrika. Tamaduni nyingi za Afrika ziliendela bila maandishi hadi juzi au hata leo. Habari zetu kuhusu utamaduni wa Zimbabwe Kuu au kuhusu uenezaji wa Wabantu hutegemea arkiolojia kwa kiasi kikubwa sana.

Hivyo arkiolojia huongeza ujuzi wetu kwa kufunua ushahidi wa nyakati za kale; wakati uleule kazi ya arkiolojia inahatarisha ushahidi huo kwa sababu kazi yake huondoa hifadhi ya udongo. Katika karne za kwanza za arkiolojia mabaki mengi ya tamaduni za kale yameharibika kutokana na kufunuliwa kwao. Kuepukana na tatizo hilo ni jukumu muhimu ya arkiolojia ya kisasa.

[hariri] Viungo

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Akiolojia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Akiolojia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -