Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Dini - Wikipedia

Dini

Kutoka Wikipedia

Nembo za Kidini:  1.: Ukristo - Uyahudi - Uhindu - Nyota ya Baha'i 2.: Uislamu - Msalaba wa Kikelti - Falsafa ya China-Korea - Shinto 3.: Ubuddha - Usikhi - Ujaini - Ujaini 4.: Ayyavali - Upagani mpya - Msalaba wa chuma - Msalaba wa Kislavoni
Nembo za Kidini:
1.: Ukristo - Uyahudi - Uhindu - Nyota ya Baha'i
2.: Uislamu - Msalaba wa Kikelti - Falsafa ya China-Korea - Shinto
3.: Ubuddha - Usikhi - Ujaini - Ujaini
4.: Ayyavali - Upagani mpya - Msalaba wa chuma - Msalaba wa Kislavoni

Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya watu pamoja na mafundisho kuhusu yale wanayoangalia ama kusadiki, yaani kiroho au kuhusiana na Mungu; maisha na uumbaji.

Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa; katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi gani kushiriki katika jumuiya za waumini.

Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani au jumuiya za kidini.

Yaliyomo

[hariri] Dini kama jumuiya kubwa

Dini kwa maana hiyo yenye wafuasi wengi duniani ni:

Pamoja na hizi kuna dini mbalimbali zinazojulikana tangu karne nyingi duniani hata kama idadi ya wafuasi si kubwa sana kwa mfano

Kuna tena imani ambazo zinafanana kati yao kwa namna fulani lakini mara huhesabiwa kama imani mbalimbali za pekee mara huhesabiwa kama kundi la dini zenye misingi ya pamoja kama matawi ya imani moja. Zikitazamiwa pamoja idadi ya wafuasi ni kubwa kiasi lakini zikihesabiwa moja-moja idadi ya wafuasi si kubwa sana, kama vile:

  • Dini asilia za Kiafrika
  • Dini asilia za Kichina
  • Ushamani

[hariri] Dini au Falsafa?

Hasa Asia ya Mashariki zimetokea mafundisho ambayo mara huhesabiwa kati ya dini mara kati ya falsafa. Mifano yake ni

  • Mafundisho ya Konfutse (Confucius)
  • Utao

Wafuasi wao mara nyingi hufuata pia dini zingine kama vile Ubuddha au Ukristo.

[hariri] Dini mpya

Historia inajua pia dini zilizotokea mara kwa mara katika nchi mbalimbali. Mfano wa dini iliyoanzishwa katika karne ya 19 na kusambaakote duniani ni Ubaha'i. Kuna mifano mingi mingine. Si rahisi kuzitaja zote.

  • Kundi la "Scientology" ni mfano wa kundi dogo lililoangaliwa sana kwa sababu wafuasi kadhaa ni watu wanaojulikana Marekani na Ulaya kutokana na filamu au magazeti.
  • Lakini miendo mipya yenye wafuasi wengi zaidi huko China kama Falungong haikuangaliwa ipasavyo kwa sababu wafuasi wake ni mbali zaidi na waandishi wa habari.
  • Rastafari ilianzishwa kama mwendo unaohesabiwa mara kama tawi al Ukristo mara kama dini mpya kati ya wakazi wa Jamaika wenye asili ya Kiafrika tangu miaka ya 1930. Kupitia wapenzi wa muziki ya Jamaika imejulikana sana duniani. Jina lake na desturi kadhaa zimetumiwa kama mwendo wa kiutamaduni hata katika sehemu zingine za dunia hara kama idadi ya wafuasi wa kidini ni ndogo.
  • Miendo ya kidini inayokua katika sehemu mbalimbali za dunia mara nyingi hazijulikana hasa zikisambaa kati ya wasemaji wa lugha moja au katika sehemu fulani ya nchi moja tu. Mfano wake ni Dini ya Musambwa katika Kenya ya Magharibi tangu miaka ya 1940.

Zaidi ya hayo kuna miendo yenye tabia za kidini zisizokubaliwa kama ni dini au la kama vile New Age au Yoga.

Dini kwa kipindi kirefu cha maisha ya mwanadamu imekuwa kitovu cha ustaarabu wa jamii husika. Hivyo kadri jamii inavyobadilika ndivyo mambo mengi huongezwa ama kutolewa katika mapokeo yake ili hali kuakisi mazingira ya nyakati.

Katika wakati wa sasa, kumekuwepo kwa jitihada mbali mbali zinazopokea na kuchunguza misingi ya Dini na maisha katika sura ya kisomi na hata kiudadisi.

[hariri] Elimu ya Dini

Kuna Masomo mbalimbali amabayo huangalia na kuchunguza dini kwa kutumia mbinu za kitaaluma. Kati ya hizo ni:

  • Theolojia ni matumizi ya mbinu za kiuanazuoni ndani ya dini fulani, kwa mfano theolojia ya kikristo, ya kiislamuu, ya kiyahudi n.k.
  • Falsafa ya dini inajaribu kutazama muundo wa fikra na mafundisho ya kidini. Inatumia mbinu na maswali ya falsafa ikitazama maswali kama: - je tunaweza kusema juu ya Mungu namna gani? - kuna maisha au uhai kupita kifo? - jinsi gani tunaweza kujua habari za mambo yajayo, maisha ya milele, asili na lengo la dunia?
  • Elimu ya dini inatazama dini mbalimbali na kuzilinganisha: jinsi zinavyobadilika, jinsi ibada zao zinaendelea, jinsi jumuiya zao zinakua au kupungua, nafasi ya dini katika maisha ya jamii n.k.
  • Somo la takwimu ya dini linajaribu kuhesabu idadi ya wafuasi wa dini mbalimbali.
  • saikolojia ya dini inajaribu kuchunguza jinsi gani aina mbalimbali za imani zinahusiana na aina za roho za kibinadamu.
  • ulinganisho wa dini inatazama hasa mafundisho na hali halisi ya dini mbalimbali jinsi zinavyofanana au kutofautiana: kwa mfano fundisho la Mungu mmoja katika Uyahudi-Ukristo-Uislamu-Uhindu; au fundisho la kuona kiroho katika umistiki (Ukristo), kabbala (Uyahudi), usufi (Uislamu), tantra (Uhindi, Ubuddha).
  • Ukosoaji wa dini uko karibu na falsafa ya dini ukiwa na mwelekeo wa kuliza maswali, kutamka wasiwasi, kuchunguza madai ya matamshi ya dini mbele ya misingi za akili ya kibinadamu
Lugha nyingine


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -