Ukosoaji wa dini
Kutoka Wikipedia
Ukosoaji wa dini ni mtindo wa kitaalamu wa fikra na mbinu zinazotaka kuchungulia madai katika matamshi ya dini, mafundisho yake na hali halisi ya dini mbele ya misingi ya akili ya kibinadamu.
Ukosoaji wa dini hutazama dini bila kukubali ukweli wake kama matamshi, mawazo na maandiko ya kibinadamu.
Kuna aina na ngazi nyingi za ukosoaji kama vile:
- kuanzia kwenye wasiwasi kama mapokeo na desturi ni za kweli au kama watumishi wa dini waliongeza au kuacha sehemu za ujumbe wa kidini
- wasiwasi kama akili na imani ya kidini zinaweza kwnda pamoja
- uhusiano wa karibu kati ya mahitaji ya jamii, siasa au uchumi na mabadiliko katika dini
- imani ya kwamba dini ni itikadi ya kibinadamu kama mawazo yote mengine
- ukosoaji wa mafundisho ya kale yasiyolingana na wakati lakini yapo katika amri za kimsingi za dini mbalimbali
na mengi mengine.
Ukosoaji wa dini unapatikana hata ndani ya jumuiya za kidini kwa namna mbalimbali:
- mafundisho ya Biblia pia ya Korani yana ukosoaji wa dini za mataifa za miungu mingi
- Ubudha ni aina ya dini isiyohitaji dhana ya Mungu
- Uislamu na Uyahudi zote zilikuwa na wafuasi ambao hawakuweza kuamini tena mafundisho ya imani lakini wamejitazama bado kama Waislamu au Wayahudi kwa sababu waliona jumuiya hizi ziko kijamii hata bila imani yenyewe. Huwa wanaangaliwa kama wazushi au wasaliti lakini walijitokea tena.
- Ukosoaji mkali katika Ulaya ulianzishwa mara nyingi na watu wenye elimu ya kidini ya Ukristo kama vile Feuerbach na Nietzsche