Mungu
Kutoka Wikipedia
Mungu ni jina linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu.
Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona Umungu kwa jinsi ulivyo au unavyofirika haukubali mgawanyiko. Hasa Waisraeli/Wayahudi, Wakristo/Ukristo na Waislamu/Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote.
Kumbe dini nyingine zinakubali uwepo wa miungu mbalimbali (wawili au zaidi).