Malta
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: L-Innu Malti | |||||
Mji mkuu | Valletta |
||||
Mji mkubwa nchini | Birkirkara | ||||
Lugha rasmi | Kimalta, Kiingereza | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri Edward Fenech Adami Lawrence Gonzi |
||||
Uhuru Kutoka Uingereza Jamhuri |
21 Septemba 1964 Desemba 13, 1974 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
316 km² (ya 185) 0.001 |
||||
Idadi ya watu - Novemba 2005 kadirio - 2005 sensa - Msongamano wa watu |
404,039 (ya 166) 404,039¹ 1,282/km² (ya 4) |
||||
Fedha | Lira ya Malta (Lm) (Euro kuanzia Januari 2008) ( MTL ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .mt 2 | ||||
Kodi ya simu | +356 |
Malta ni nchi ndogo kwenye funguvisiwa katika Mediteranea. Malta iko 93 km kusini ya kisiwa cha Sisilia (Italia), upande wa mashariki wa Tunisia na kaskazini ya Libya.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Funguvisiwa vya Malta ina visiwa saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta (246 km²)na Gonzo (70 km²). Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu ndicho Comino (3 km²). Vingine ni vidogo havina watu. Jumla la eneo ni 316 km².
Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililounganisha Afrika na Ulaya na kukatwa na kupanda kwa uwiano wa bahari tangu mwaka 11,000 KK. Sehemu za juu ni vilima vya Dingli Cliffs vyenye kimo cha 245 m juu ya UB.
Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa maji matamu. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari kwa njia ya osmosi vinatengeneza maji ya kunywa. Maji machafu husafishwa na mvua kukusanywa.
[hariri] Wakazi na Miji
Kwa jumla kuna wakazi 404,039 (wa kiume 200,715 (49.7%) na wa kike 203,324 (50.3%)). Msongamano wa watu ni 1,282 kwa kilomita ya mraba amabo ni msogamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya.
Miji mikubwa zaidi ni : Birkirkara (wakazi 21,676), Qormi (wakazi 18,230), Mosta (wakazi 17,789), Zabbar (wakazi 15,030), Victoria (wakazi 12,914) na San Gwann (wakazi 12,346). Mji mkuu Valletta una wakazi 7,173 pekee.
Karibu wakazi wote ni Wakatoliki.
[hariri] Lugha na utamaduni
Lugha ya Kimalta ni lugha ya pekee. Asili yake ni lahaja ya Kiarabu iliyopokea maneno mengi ya Kiitalia, Kiingereza, Kihispania na Kifaransa. Ni lugha ya pekee ya Kisemiti inayoandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini.
Lugha rasmi ya pili ni Kiingereza kutokana na miaka 150 ya ukoloni wa Uingereza. Wamalta wengi sana huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani Italia.
[hariri] Historia
Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna maghofu ya hekalu ya mwaka 3200 KK. Baadaye fungivisiwa ilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma. Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliokolewa baada baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini (Mdo 27,39 nk).
Waarabu walivamia kisiwa mwaka 870 na kukitawala hadi 1091. Baadaye ilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, baadaye na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Roma-Ujerumani.
Tangu 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa wamisalaba wa chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu. Wamisalaba hawa walikuwa mabwana wa visiwa hadi Napoleoni aliyeteka Malta mwaka 1799 safarini kwenda Misri. Uingereza ilitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa. Ikatawala Malti hadi uhuru wake tar. 21 Septemba 1964.
13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola. 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.
[hariri] Viungo vya Nje
Makala hiyo kuhusu "Malta" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Malta kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |