Jumuiya ya Madola
Kutoka Wikipedia
Lugha rasmi | Kiingereza |
Katibu Mkuu | Don McKinnon (tangu 1999) |
Chanzo chake | mw. 1926 kama jumuiya ya "Kibritania", tangu 1949 kama Jumuiya ya Madola ya kisasa |
Madola wanachama | 53 |
Makao Makuu | Westminster, London |
Mtandao | thecommonwealth.org |
Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake.
Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza ambayo ilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi.
Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani (watu 1,800,000) huishi katika nchi wanachama za Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee.