Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Msumbiji - Wikipedia

Msumbiji

Kutoka Wikipedia

República de Moçambique
Jamhuri la Msumbiji
Bendera ya Msumbiji Nembo la Msumbiji
Lugha ya Taifa Kireno
Mji Mkuu Maputo
Aina ya Serikali Jamhuri
Rais Armando Guebuza
Waziri Mkuu Luisa Diogo
Eneo 801.590 km²
Wakazi 19.406.703 (Julai 2005)
Wakazi kwa km² 24
JPT/ Mkazi 233 US-$ (2004)
Uhuru kutoka Ureno tar. 25.06.1975
Pesa Metical (MZM)
Wakati UTC +2h
Wimbo ya Taifa (inaangaliwa upya)
Namba ya simu ya kimataifa +258
Msumbiji katika Afrika

Msumbiji (Kireno: Moçambique) ni nchi ya Afrika ya Kusini-Mashariki. Sikukuu ya Taifa ni tar. 25.06., kutokana na uhuru mwaka 1975.

Msumbiji iko ufukoni wa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Uswazi. Upande wa mashariki kuna kisiwa cha Madagaska ng'ambo ya mlango bahari wa Msumbiji.

Jina la nchi imetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kireno: Ilha de Moçambique) iliyokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.

Ramani ya Msumbiji
Ramani ya Msumbiji

[hariri] Jiografia

Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya sehemu ya kusini ya nchi lakini kwenda kaskazini upana wake inapungua. Nyuma ya tambarare nchi inapanda hadi kufika uwiano wa tambarare ya juu ya Afrika ya Kusini. Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.

Mito iko mingi ikiwa mkubwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani na Tanzania, Save na Limpopo. Ziwa la Nyassa ni sehemu ya mpaka na Malawi.

Umbo la eneo la nchi ni ndefu sana ni kilomita 2000 kutoka mpaka na Tanzania upande wa kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini. Pwani la Bahari Hindi ina urefu wa 2.470 km

Miji mikubwa zaidi ni Maputo (wakazi 1.191.613), Matola (wakazi 543.907) na Beira (wakazi 530.706).

[hariri] Historia

Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wavindaji Wasan. Katika karne za kwanza BK wahamiaji Wabantu walifika wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Haujulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.

Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.

Taarifa za kwanza ya kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.


Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Msumbiji" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Msumbiji kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Lugha nyingine


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -