Botswana
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Pula (Mvua) | |||||
Wimbo wa taifa: Fatshe leno la rona (Nchi hii nzuri ibarikiwe) |
|||||
![]() |
|||||
Mji mkuu | Gaborone |
||||
Mji mkubwa nchini | Gaborone | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza (rasmi), KiTswana (kitaifa) | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri ya kibunge Festus Gontebanye Mogae |
||||
Uhuru Kutoka Uingereza |
Septemba 30, 1966 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
600,370 km² (46th) 2.5% |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
1,765,000 (147th) 2.7/km² (223rd) |
||||
Fedha | Pula (BWP ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+2) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .bw | ||||
Kodi ya simu | +267 |
Botswana ni nchi iliyoko Kusini mwa Afrika. Jina rasmi ni Jamhuri ya Botswana. Mji mkuu wa Botswana ni Gaborone.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Botswana haina pwani ya bahari yoyote. Imepakana na Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia. Kuna pia feri ya moja kwa moja kati ya Botswana na Zambia kuvuka mto Zambezi.
Jangwa la Kalahari linafunika theluthi mbili za eneo la Botswana. Moja ya maeneo muhimu nchini Botswana ni delta ya mto Okavango. Delta ya Okavango ni delta kubwa kabisa duniani, maana yake mdomo wa mto si baharini bali kwenye nchi kavu, maji yakiishia jangwani.
[hariri] Utamaduni
Watu wa Botswana hujiita "Batswana. Kuna wakazi takriban milioni 1.6. Kwa sababu nchi ni kubwa songamano la watu ni watu ni kilometa za mraba 2.7 pekee. Idadi hiyo ndogo imetokana na sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa ni jangwa.
Lugha inayotumika na wakazi walio wengi ni Setswana (Kitswana) pamoja na Kiingereza.
Botswana imekuwa na mfumo wa demokrasia kwa miaka mingi ikiwa viongozi ambao huchaguliwa kwa kura ya wananchi wote.
Rais wa jamhuri ni Festus Mogae.
[hariri] Uchumi
Uchumi wa Botswana umekuwa imara kwa miaka mingi na hali ya maisha imeendelea kuwa bora kila mwaka tangu uhuru .
Utajiri wa nchi unatokana hasa na migodi ya almasi, pamoja na machimbo ya shaba na minerali kama vile chumvi. Watalii wanaongeza pato la taifa hasa kwa sababu ya uzuri wa delta ya Okavango.
Fedha ya Botswana huitwa Pula (yaani mvua). Ina thebe (="ngao") 100.
[hariri] Viungo vya nje
Nchi za Afrika | ![]() |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |