Niger
Kutoka Wikipedia
Kwa maana nyingine ya neno "Niger" tazama makala ya Niger (maana)
|
|||||
Wito la taifa: Fraternité, Travail, Progrès (Undugu, Kazi, Maendeleo) |
|||||
Wimbo wa taifa: La Nigerienne | |||||
Mji mkuu | Niamey |
||||
Mji mkubwa nchini | Niamey | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa | ||||
Serikali | Jamhuri Tandja Mamadou Hama Amadou |
||||
Uhuru imetangazwa |
kutoka Ufaransa 3 Agosti, 1960 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
1,267,000 km² (ya 22) 0.0002% |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
11,665,937 (ya 69) 9/km² (ya 175) |
||||
Fedha | Franki ya CFA (XOF ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+1) (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .ne | ||||
Kodi ya simu | +227 |
Niger ni nchi ya Afrika ya Magharibi. Imepakana na Algeria na Libya upande wa kaskazini, Mali na Burkina Faso upande wa magharibi, Chad upande wa mashariki na Nigeria pamoja na Benin upande wa kusini. Mji mkuu ni Niamey katika kusini ya nchi.
Niger haina pwani na bahari yoyote. Ni sehemu ya kanda la Sahel yaani sehemu kubwa ya nchi ni yabisi, kaskazini yake ni yabisi sana ikiwa jangwa la Sahara, na nchi ya rutba iko kusini kabisa tu karibu na mto wa Niger.
Mipaka imechorwa wakati wa ukoloni wa Ufaransa ikiunganisha watu wa utamaduni tofauti kama vile Tuareg wa Sahara, wahamiaji Wafulani na Wakanuri wa eneo la Sahel na wakulima wa kusini kama Wasonghai na Wahaussa
Tofauti hizi kubwa zilileta kipindi cha ugomvi wa makabila uliopoa tena baada ya mwaka 2000. Tatizo kubwa la nchi ni vipindi vya ukame na njaa vinyvyorudia mara kwa mara.
Wakazi walikadiriwa kuwa karibu milioni 12 katika mwaka 2005. Idadi kubwa wako kusini. Walio wengi kabisa ni wafuasi wa Uislamu waliokadiriwa kuwa 94-97% za wananchi; sehemu yao wanasemekana kuchanganya Uislamu na imani asilia.
Makala hiyo kuhusu "Niger" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Niger kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |