Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Benin - Wikipedia

Benin

Kutoka Wikipedia

République du Bénin
Jamhuri ya Benin
Flag of Benin Nembo ya Benin
Bendera Nembo
Wito la taifa: Fraternité, Justice, Travail
(Kifaransa: Ushirikiano, Haki, Kazi)
Wimbo wa taifa: L'Aube Nouvelle
Lokeshen ya Benin
Mji mkuu Porto Novo, Cotonou1
6°28′ N 2°36′ E
Mji mkubwa nchini Cotonou
Lugha rasmi Kifaransa
Serikali Jamhuri ya kidemokrasia
yenye vyama vingi

Yayi Boni
Uhuru
kutoka Ufaransa
1 Agosti, 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
112,620 km² (101st)
1.8
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
7,862,944 2 (89th)
69.8/km² (102nd 3)
Fedha CFA franc (XOF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+ 1)
(UTC)
Intaneti TLD .bj
Kodi ya simu +229
1.) Mji wa Cotonou ni makao makuu ya serikali.
2.) Angalizo: Makadirio kwa nchi hiyo yamehesabu pia maafa ya ziada yaliyosababishwa na UKIMWI. Hii ingeweza kusababisha takwimu tofauti na itarajiwayo
3.) Mwaka wa makadirio ni 2005.

Jamhuri ya Benin ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Zamani iliitwa Dahomey. Inapakana na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini, nchi ya Togo upande wa Magharibi, nchi ya Nigeria upande wa Mashariki na nchi za Burkina Faso na Niger upande wa Kaskazini. Haihusiani na Mji wa Benin (Benin City) wala na Ufalme wa Benin wa karne ya 19.

Yaliyomo

[hariri] Historia

Sherehe na ngoma kule Abomey, 1908
Sherehe na ngoma kule Abomey, 1908

Ufalme wa Dahomey ulianzishwa katika nchi ya kisasa ya Benin. Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi. Kulikuwa na utajiri mkubwa kwa sababu ya biashara na Wazungu, hasa Wareno na Waholanzi waliofika kuanzia mwisha wa karne ya 15. Pwani ya Benin ilijulikana kama Pwani ya Watumwa. Biashara ya watumwa iliendelea kwa karne tatu mpaka mwaka wa 1885.

Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899, na walipata uhuru 1 Agosti, 1960. Mpaka mwaka wa 1972 makundi mbalimbali walipigania vita, mpaka Wakomunisti walianza kutawala na kiongozi wao Mathieu Kérékou. Nchi ilipewa jina lipya, yaani Jamhuri ya Benin, mwaka wa 1975. Tangu miaka ya 80 ya karne ya 20, nchi ilifuata mfumo wa soko huru. Kérékou alikuwa Rais hadi 1991, halafu tena 1996-2006. Katika uchaguzi wa Machi 2006, Yayi Boni alipata urais aliouanza 6 Aprili 2006.

[hariri] Siasa

Main article: Siasa ya Benin

Template:Siasa ya Benin Bunge la Benin lina viti 83. Huchaguliwa kila mwaka wa nne. Rais ni mkuu wa serikali na wa nchi, naye huchaguliwa kila mwaka wa tano. Mgombea urais asiwe na umri wa miaka zaidi ya sabini.

[hariri] Utawala

Main article: Utawala wa Benin

Kuna majimbo 12, nayo ni:

  • Alibori
  • Atakora
  • Atlantique
  • Borgou
  • Collines
  • Donga
  • Kouffo
  • Littoral
  • Mono
  • Ouémé
  • Plateau
  • Zou

[hariri] Jiografia

Nchi ya Benin iko kati ya Mto wa Niger upande wa Kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini. Haina milima mirefu. Idadi kubwa ya watu wanaishi katika tambarare za Kusini ambapo miji mikubwa ya Benin iko, pamoja na miji ya Porto Novo na Cotonou. Sehemu za Kaskazini ni kavu hasa.

Nchi ya Benin inapata majira mawili ya mvua, Aprili-Julai na Septemba-Novemba. Pia kuanzia mwezi wa Desemba, kuna upepo ulioitwa harmattan, nao huleta vumbi na baridi wakati wa usiku.

[hariri] Uchumi

Uchumi wa Benin hauna nguvu sana, na hutegemea hasa kilimo, mazao ya pamba na biashara ndogondogo.

[hariri] Demografia

Picha kutoka kijiji cha Benin
Picha kutoka kijiji cha Benin

Kuna makabila mbalimbali ambo wanaongea lugha tofauti sana, k.m. Kihausa, lugha za Kisonghay, lugha za Kimande na lugha za Kifulani. Kabila kubwa kabisa ni Wafon.

[hariri] Marejeo

  • Adam, Kolawolé Sikirou and Michel Boko (1983), Le Bénin. SODIMAS, Cotonou and EDICEF, Paris.

[hariri] Viungo ya nje


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Lugha nyingine


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -