Shelisheli
Kutoka Wikipedia
|
|||
Wito: Finis Coronat Opus. (Kilatini "Matokeo ni taji la kazi") |
|||
Lugha rasmi | Seselwa, Kiingereza, Kifaransa | ||
Mji Mkuu | Victoria | ||
Serikali | Jamhuri | ||
Rais | James Alix Michel (tangu tar. 14 Aprili, 2004) | ||
Eneo | 455 km² | ||
Idadi ya wakazi | 80.832 (Julai 2004) | ||
Wakazi kwa km² | 177 | ||
Uhuru | 29 Juni, 1976 (kutoka Uingereza) | ||
Pesa | Rupia ya Shelisheli | ||
Wakati | UTC +4 | ||
Wimbo la taifa | Koste Seselwa | ||
Shelisheli ni funguvisiwa na jamhuri katika Bahari Hindi mbele ya mwabao wa mashariki ya Afrika upande wa kaskazini wa Madagaska na Mauritius na mashariki wa Komoro.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Shelisheli ina visiwa 115; 32 kati ya hizo ni visiwa vikubwa kidogo vyenye milima vingine ni vidogo huitwa "Visiwa vya nje".
Wakazi wengi huishi kwenye visiwa karibu na Mahé ndivyo hasa Praslin na La Digue. Visiwa hivi vina milima inayofikia hadi 900 m juu ya UB. Ndio mkubwa ni Morne Seychellois yenye mita 905 juu ya UB.
Hali ya hewa ni ya kitropiki ikiwa halijoto iko kati ya 24 °C na 30 °C. Kiasi cha mvua ni kati ya 2.880 mm (huko Mji Mkuu Victoria na 3.550 mm mlimani.
[hariri] Wakazi
Wakazi kwa jumla ni chotara wenye damu ya Madagaska, Afrika bara na Ulaya. Licha ya hayo kuna vikundi vidogo vya Wazungu, Wachina na Wahindi watupu.
Walio wengi ndio Wakristo Wakatoliki (90%), idadi ndogo ndio Waprotestant, wengine wachache ni Wahindu, Wabuddha au waislamu.
[hariri] Historia
Hakuna uhakika kuhusu wakazi wa kwanza. Inaaminika ya kwamba ndio mabaharia na wafanyabiashara Waarabu. Taarifa ya kwanza imepatikana kutoka kwa Wareno waliozunguka hapa kuanzia mwaka 1505. Kwa karne moja na nusu meli au jahazi zilipitia Shelisheli tu kwa kusudi la kuchota maji ya kunywa auch kukusanya matunda bila kuanzisha makao ya kudumu. Majambazi wa baharini walipenda kujificha Shelisheli.
Ndio Ufaransa iliyojenga vituo vya kwanza vya kudumu mwaka 1756. Wafaransa waliita visiva "Seychelles" kwa heshima ya waziri wa Kifaransa wa siku zile Jean Moreau de Sechelles. Walowezi wao walianzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara wakitumia watumwa kutoka Madagaska na Afrika bara kwa ajili ya kazi yenyewe.
Tangu mwaka 1814 visiwa vilikuwa chini ya Uingereza. Shelisheli zilikuwa zikitawaliwa pamoja na Mauritius. Mwaka 1903 visiwa vilipewa cheo cha koloni pekee na Mauritius. Waingereza walivumulia walowezi na utamaduni wa Kifaransa visiwani.
Mwaka 1970 Shelisheli walipata Uhuru. Katiba ya kwanza ilifuata mfano wa Uníngerezeza lakini mw. 1979 katiba mpya ilileta mfumo wa chama kimoja. Tangu 1993 katiba ilisahihishwa tena ikiruhusu vyama vingi vya kisiasa. Chama kilichopata kura nyingi ndicho SPPF (Seychelles People's Progressive Front).
[hariri] Uchumi
Biashara ya shelisheli ni hasa utalii. Mnamo asilimia 30 za wafanyakazi wote wamo katika utalii. Biashara hii inaingiza 70% ya pato la taifa. Pamoja na utalii uvuvi na kilimo ni muhimu pia.
[hariri] Viungo vya nje
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |