Rupia
Kutoka Wikipedia
Rupia ni jina la pesa inayotumika leo India na nchi mbalimbali za Asia. Ni pia jina la pesa iliyowahi kutumika Afrika ya Mashariki na nchi mbalimbali.
[hariri] Jina na historia
Neno "rupia" limetokana na lugha ya kihindi ya kale "rūp" au "rūpā" linalomaanisha "fedha". Katika lugha ya Sanskrit "rupyakam" (रूप्यकम्) inamaanisha sarafu ya fedha. Hii ni asili ya "Rūpaya" iliyotumika katika India kama sarafu yenye gramu 178 za fedha tangu 1540 . Rupia moja ilikuwa na 16 Anna, 64 Paisa au 192 Pai.
[hariri] Pesa ya kisasa
Leo hii nchi zifuatazo zinatumia jina la Rupia (Rupiah, Rupee: ₨) kwa pesa zao:
[hariri] Pesa ya kihistoria
Rupia ilikuwa kihistoria pesa ya nchi na maeneo yafuatayo:
- Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
- Afrika ya Mashariki ya Kiingereza
- Zanzibar
- Kwenye eneo la India ya leo katika koloni za nchi zifuatazo: Denmark, Ufaransa na Ureno, pia katika madola mbalimbali ya Kihindi kabla ya ukoloni na kabla ya uhuru kama vile Hyderabad.
- Katika nchi jirani za India kama vile Bhutan, Burma, Sri Lanka, Afghanistan
- Katika maeneo ya Ghuba ya Uajemi
- Somalia ya Kiitalia
- huko Indonesia wakati wa uvamizi wa Japan 1940-1945