Pesa
Kutoka Wikipedia
Pesa ni chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya watu. Pesa yenyewe haina faida haitoshelezi mahitaji ya kibinadamu ila imekubaliwa katia jamii kama njia ya kujipatia mahitaji mengine.
Kuna maneno mengine kwa pesa kama vile hela, fedha au sarafu.
[hariri] Historia ya pesa
Kiasili watu walibadilishana vitu kwa mfano ng'ombe mmoja kwa mbuzi kadhaa au mazao kwa samaki nk. Baadaye imeonekana ya kwamba itasaidia zaidi kama kiwango fulani inapatikana kwa vitu vyote.
Metali zilizokuwa haba zilitumiwa kama kipimo hiki kwa mfano dhahabu, fedha au shaba. Vilipimwa kufuatana uzito. Hatua iliyofuata ilikuwa kutumia vipande vya metali hizi vilivyogongwa mihuri halafu hapakuwa na lazima ya kuvipima kimoja-kimoja. Inavyojulikana Wachina walikuwa watu wa kwanza waliochukua hatua hii katika milenia ya 2 KK. Hii ilikuwa mwanzo wa sarafu.
Pesa hutolewa na serikali ya nchi au na taasisi kama benki kuu inayofanya kazi hii kwa niaba ya serikali. Mwanzoni sarafu ilikuwa sawa na kiasi fulani cha dhahabu au fedha.
Hatua nyingine ilikuwa kutolewa kwa pesa ya karatasi au benknoti zilizoahidi kumpatia mtu yeyote kiasi kilichoandikwa kwa dhahabu au fedha yenyewe. Kwa muda mrefu benki kuu zilikuwa na hazina ya dhahabu iliyolingana na kiasi cha benknoti zilizochapishwa.
Katika karne ya 20 nchi zote zilifanya hatua ya kuacha makadirio ya dhahabu kwa sababu thamani ya bidhaa katika jamii ilipita kiasi cha dhahabu iliyopatikana. Siku hizi jumla ya pesa inayotolewa inatakiwa kulingana na thamani ya rasilmali ya taifa fulani.
Pale ambako serikali inachapisha benknoti kushinda kiwango hicho thamani ya pesa inashuka na mfumko wa bei inatokea.
[hariri] Viungo vya Nje
- Linguistic and Commodity Exchanges by Elmer G. Wiens. Examines the structural differences between barter and monetary commodity exchanges and oral and written linguistic exchanges.
Makala hiyo kuhusu "Pesa" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Pesa kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |