Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Jangwa - Wikipedia

Jangwa

Kutoka Wikipedia

Matuta ya mchanga katika Sahara ya Libya
Matuta ya mchanga katika Sahara ya Libya
Nguzo za mwamba katika Jangwa la Australia
Nguzo za mwamba katika Jangwa la Australia

Jangwa ni eneo pakavu penye mvua au usimbishaji kwa ujumla chini ya 250 mm kwa mwaka. Kutokana na ukavu kuna mimea michache tu pia wanyama wachache. Wanyama walioko hufanya shughuli zao hasa wakati wa usiku.

Wakati mwingine maeneo huitwa jangwa ambayo ni makavu kutokana na baridi kali.

Yaliyomo

[hariri] Aina za maeneo makavu: jangwa na mibuga

Maeneo makavu yanaweza kutofautishwa kuwa yabisi sana (en: extremely arid) pasipo na usimbishaji kwa muda wa miezi 12 mfululizo (maana yake hakuna mvua kila mwaka), yabisi (en: arid) pasipo na usimbishaji zaidi ya 250 mm kwa mwaka, nusu yabisi (en:semiarid) penye usimbishaji kati ya 250 and 500 mm kwa mwaka. Maeneo yabisi sana na maeneo yabisi ni jangwa. Maeneo nusu yabisi pana manyasi huitwa mbuga.

[hariri] Athari ya uvukizaji

Kiasi cha usimbishaji peke yake hakitoshi kila mahali kutofautisha maeneo makavu. 200 mm za mvua katika eneo la joto zitasababisha eneo kuonekana kama jangwa kabisa kwa sababu kiasi kikubwa cha maji yale kidogo yanayoneshewa hupotea kutokana na uvukizaji. Kuna mifano ya kwamba eneo penye kiasi kilekile cha 200 mm halionekani kuwa jangwa tayari kwa sababu kutokana na halijoto na mawingu (hata yasiponyesha mvua) kiasi kidogo cha maji yanavukiza.

Kama uvukizaji unapita kiasi cha mvua hata eneo penye mvua zaidi ya 250 mm inaonekana kama jangwa.

[hariri] Aina za jangwa

Mara nyingi jangwa hutofautishwa kutokana na uso lake:

  • Jangwa la mchanga — uso lake huonyesha hasa mchanga. Mchanga umetokea kutokana na mmomonyoko wa changarawe na kokoto kama mawe haya ni hasa ya shondo. Punje ndogo za mchanga husukumwa na upepo na kutokea kama matuta makubwa ya mchanga. Jangwa la mchanga ni mahali pagumu mno kwa maisha ya kila aina. Mfano bora ni jangwa la Rub al-Khali katika Uarabuni Saudi. Sahara ina pia sehemu za jangwa la mchanga.
Jangwa baridi la mawe la Ladakh kwenye milima ya Himalaya
Jangwa baridi la mawe la Ladakh kwenye milima ya Himalaya
  • Jangwa la changarawe — uso lake huonyesha hasa changarawe. Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au miamba - punje ndogo zaidi zimeshapulizwa mbali na upepo. Hii ni sababu ya majangwa mengi kuwa na maeneo ya mchanga na changarawe yanayobadilishana. Changarawe hupatikana pia pale ambako zamani barafuto zilisaga mawe na kuzisukuma mbele ya barafu zao pale zilizobaki. Ni ajabu kutafakari ya kwamba sehemu fulani ilikuwa ya barafuto tukisimama leo mahali penye joto kali lakini mabadiliko ya hali ya hewa yalileta baridi au joto kila sehemu ya dunia yetu katika mamilioni ya miaka iliyopita.
  • Jangwa la mawe — uso lake huonyesha miamba na mawe makubwa. Maana yake hapo udongo wote mwenye rutba na mchanga vimeshapulizwa mbali na mwamba umebaki. Athira za joto na baridi zinaweza kupasua mwamba. Mmomonyoko wa upepo hutokea.
  • Jangwa la chumvi — mara nyingi penye beseni yabisi za mashapo bila njia ambako maji ya mvua (au mto) yanaweza kutoka. Maji yote huvukiza na kuacha chumvi yake katika udongo. Kiasi cha chumvi kinaendelea kuongezeka polepole katika udongo wa beseni hizi.

[hariri] Maji

Jangwa ni eneo kavu lakini maji hutokea.

[hariri] Maji ya chini

Mara nyingi kuna maji chini ya ardhi. Pale ambako maji haya si chini mno mimea inaweza kuyafikia kwa mizizi yao. Mahali kadhaa chemchemi hutokea. Sehemu kama hizi zinaonekana kama oasisi penye miti, wakati mwingine hata na bwawa. Mahali pengine wakazi wa jangwa wamechimba kisima kirefu pasipo na mimea kinachosaidia maji ya watu na wanyama hasa wa misafara.

[hariri] Maji ya mvua

Mvua ikionyesha unaweza kutokea kwa wingi. Maji yake hukusanyika katika mabonde na kutokea kama mto wa muda. Kuna mifano mingi ya wasafiri jangwani waliokufa kwa sababu walipiga kambi katika bonde penye kivuli lakini walizama kwa sababu mto mkali ulijitokeza kwa ghafla kutokana na mvua ulionyesha katika umbali mkubwa.

Sehemu nyingine mvua husababisha kutokea kwa mbwawa hata maziwa kwa muda.

Jangwa la Sahari jinsi lafunika Afrika ya Kaskazini yote (picha kutoka angani)
Jangwa la Sahari jinsi lafunika Afrika ya Kaskazini yote (picha kutoka angani)

[hariri] Mito inayopita jangwa

Mito kadhaa kama Nile ina maji ya kutosha ili ivuke neo la jangwa. Inawezesha maisha ya mimea, wanyama na watu katika mabonde yao.

Mito mingine inakwisha jangwani kwa sababu maji yote hupotea na kuvukiza. Mfano wake ni delta ya mto wa Okavango unaokwisha katika jangwa la Kalahari huko Botswana. Delta hii ni eneo la mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa.

Mto wa Ewaso Nyiro katika Kenya ya kaskazini kwa kawaida hukwisha katika nchi yabisi za Usamburu. Lakini kila baada ya miaka makumi kadhaa baada ya mvua kubwa sana inaendelea kuvuka jangwa la Somalia ya kusini na kufikia Bahari Hindi jinsi ilvyotokea wakati wa El-Nino 1998.


[hariri] Majangwa makubwa duniani

  • Majangwa makubwa 10 ya dunia:
Jina la jangwa Eneo (km²)
Sahara (Afrika) 9 000 000
Jangwa la Uarabuni 1 300 000
Jangwa la Gobi (Uchina / Mongolia - Asia) 1 125 000
Jangwa la Kalahari (Afrika ya Kusini) 580 000
Jangwa Kuu la Australia 414 000
Karakum (Asia) 350 000
Taklamakan (Asia) 344 000
Jangwa Namib (Namibia - Afrika) 310 000
Thar (Asia) 260 000
Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Jangwa" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Jangwa kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -