Maryland
Kutoka Wikipedia
Maryland ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani la Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, West Virginia, Delaware, Virginia na mkoa wa shirikisho la Washington DC.
Hori la Chesapeake linagawa eneo la jimbo kwa pande mbili. Mji mkuu ni Annapolis (Maryland) na mji mkubwa ni Baltimore.
Iliundwa kama koloni ya Ungereza mwaka 1634 na mkabaila Lord Baltimore aliyetumia jina la Maryland kwa heshima ya mke wa mfalme Charles I. Baltimore aliyetoka Ueire alitafuta hasa mahali kwa ajili ya Wakatoliki wasiokubaliwa katika koloni nyingine za Uingereza. Maryland ilikuwa koloni ya kwanza yenye sheria iliyokubali madhehebu yote ya kikristo.
Mji mkuu wa Washington DC ulijengwa kwenye eneo lililotengwa na eneo la Mayrland kando la mto Potomac. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani 1861-1865 Maryland ilikaa upande wa Maungano.
[hariri] Viungo vya Nje
- State of Maryland (tovuti ya serikali)
- USGS habari za Maryland
- U.S. idara ya sensa
Makala hiyo kuhusu "Maryland" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Maryland kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |