Delaware
Kutoka Wikipedia
Delaware ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani la Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, Maryland na kwa kilomita chache pia na New Jersey. Mji mkuu ni Dover lakini mji mkubwa ni Wilmington.
Jina la jimbo latokana na mto Delaware na hori la Delaware ambazo zote ziliitwa kwa heshima ya mkabaila Mwingereza De La Warr katika mnamo mwaka 1600.
Delaware ni jimbo dogo lenye eneo la 6,452 km² na wakazi 783,600 pekee. Kati ya majimbo ya Marekani ni jimbo lenye mapato ya juu kwa kila raia. Sheria zake za kodi ya mapato ni nafuu hivyo makampuni mengi yamepeleka ofisi zao hapa. Menginyevyo uzalishaji hi hasa mazao ya kilimo pamoja na ufugaji kuku.
[hariri] Historia
Ilianzishwa kama kituo cha biashara ya Sweden mwaka 1638 iliyovamiwa na Uholanzi na kuwa baadaye koloni ya Uingereza tangu 1664. Delaware ilikuwa koloni ya kwanza ya kukubali katiba mpya ya Maungano ya Madola ya Amerika baada ya uasi wa koloni 13 za Uingereza katika Amerika ya Kaskazini.
Makala hiyo kuhusu "Delaware" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Delaware kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |