Virginia
Kutoka Wikipedia
Virginia ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika mashariki ya Marekani bara. Imepakana na West Virginia, Maryland na mkoa wa shirikisho la Washington D.C. upande wa kaskazini, North Carolina na Tennessee upande wa kusini halafu Kentucky na West Virginia upande wa magharibi. Upande wa mashariki ni bahari ya Atlantiki pamoja na hori ya Chesapeake.
Mji mkuu ni Richmond (Virginia) na mji mkubwa ni Virginia Beach.
Virginia ilikuwa koloni ya Uingereza tangu kuanzishwa kwa mji wa Jamestown (Virginia) mwaka 1607. Jina la "Virginia" lamaanisha "kibikira" kwa heshima ya malkia Elisabeth I ambaye hakuolewa. Mwaka 1788 ilikuwa jimbo la kujitawala la nchi mpya ya Marekani ni moja kati ya majimbo 13 yaliyoanzisha Marekani.
Jimbo la West Virginia iliwahi kuwa sehemu ya Virginia. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Virginia iliondoka katika maungano ya madola ya Marekani ikajiunga na waasi wengine katika Shirikisho la Marekani. Wakati ule wilaya kwenye magharibi ya jimbo zilijitenga na kuwa jimbo jipya lililobaki upande wa maungano hata baada ya mwisho wa vita.
Makala hiyo kuhusu "Virginia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Virginia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |