West Virginia
Kutoka Wikipedia
West Virginia (Virginia Magharibi) ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika mashariki ya Marekani bara. Imepakana na Ohio, Kentucky, Maryland na Virginia.
Mji mkuu pia mji mkubwa ni Charleston. Jimbo lina wakazi 1,808,344 (2000) wanaokalia eneo la kilomita za mraba 62,0809.
Kabla ya 1863 eneo la jimbo lilikuwa sehemu za Virginia. Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani Virginia iliondoka katika maungano ya madola ya Marekani ikajiunga na waasi wengine katika Shirikisho la Marekani. Wakati ule wilaya za magharibi ya jimbo zilijitenga na kuwa jimbo jipya lililobaki upande wa maungano. Wilaya hizi ziliendelea kama jimbo la pekee la "West Virginia" hata baada ya mwisho wa vita.
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |