Nebraska
Kutoka Wikipedia
Nebraska ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katikati ya Marekani bara ikipakana na majimbo ya South Dakota, Iowa, Missouri, Kansas, Colorado na Wyoming.
Mji mkuu ni Lincoln na mji mkubwa jimboni ni Omaha. Jimbo lina wakazi 1,711,263 (2000) wanaokalia eneo la kilomita za mraba 200,520.
Nebraska ni hasa jimbo la kilimo cha mahindi pamoja na ufugaji wa ng'ombe.
Hali ya hewa ni majira ya joto na baridi kali. Wakati wa Julai/Agosti halijoto hufikia +30°C inayoshuka hadi -20°C wakati wa January.
Eneo la Nebraska lilitwaliwa na Marekani mwaka 1854. Baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani eneo likapewa cheo cha jimbo kamili.
Makala hiyo kuhusu "Nebraska" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Nebraska kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |