Georgia (jimbo)
Kutoka Wikipedia
Georgia ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kusini mashariki ya Marekani bara. Imepakana na Florida, Alabama, Tennessee, North Carolina na South Carolina. Upande wa kusini magharibi kuna pwani la Atlantiki.
Georgia ilikuwa kati ya koloni asilia 13 za Kiingereza katika Amerika ya Kaskazini zilizoasi dhidi ya Uingereza 1776 ikawa jimbo la Marekani 1788.
Jina la koloni asilia lilitolewa kwa heshima ya mfalme George II. wa Uingereza aliyekuwa pia mtemi wa Hannover.
Mji mkuu na mji mkubwa wa jimbo la Georgia ni Atlanta. Eneo la jimbo ni 154,077 km² na idadi ya wakazi inazidi milioni nane.
Takriban theluthi ya wakazi wana asili ya Kiafrika ni watoto wa watumwa wa kale.
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |