Iowa
Kutoka Wikipedia
Iowa ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika magharibi ya kati ya Marekani bara. Imepakana na Minnesota, Nebraska, South Dakota, Missouri na Illinois. Mto Missisippi ni mpaka wake upande wa mashariki kutazama Wisconsin na Illinois; mto Missouri ni mpapa wake upande magharibi kutazama Nebraska. Imekuwa jimbo la Marekani tangu 1846.
Mji mkuu wa jimbo na pia mji mkubwa ni Des Moines. Idadi ya wakazi wa jimbo lote hufikia watu 2,926,324 wanaokalia eneo la 145,743 km² ambalo ni hasa tambarare lenye rutba.
[hariri] Economy
Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi na kuna mashamba makubwa Iowa. Mahindi yanayolimwa hasa pamoja na soya yanalisha nguruwe na ng'ombe. Sehemu ya mazao hutumiwa kwa kutengeneza petroli ya ethanol.
Makala hiyo kuhusu "Iowa" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Iowa kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |