Washington
Kutoka Wikipedia
Washington ni kati ya majimbo ya kujitawala ya Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kaskazini magharibi ya Marekani bara. Imepakana na Oregon, Idaho na British Columbia katika Kanada. Upande wa magharibi kuna pwani la Pasifiki.
Jina la jimbo lilitolewa kwa heshima ya rais wa kwanza wa Marekani George Washington.
Mji mkuu wa jimbo ni Olympia. Hii ni mji mdogo. Miji miwili mikubwa ya jimbo ni Seattle na Spokane. Eneo la jimbo ni 184,824 km² na idadi ya wakazi inazidi milioni sita.
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |