Ohio
Kutoka Wikipedia
Ohio ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kaskazini mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, Michigan, Indiana, Kentucky na West Virginia. Upande wa kazkazini ni mpaka wa kimataifa na ng'ambo yake iko jimbo la Ontario katika Kanada. Mipaka asilia ni Ziwa Erie upande wa kazkazini na mto Ohio upande wa mashariki na kusini.
Mji mkuu pia mji mkubwa jimboni ni Columbus. Miji mingine mikubwa ni Cleveland, Cincinnati na Dayton.
Jina la Ohio limetokana na jina la Kiindio kwa mto mkubwa ulio mpaka wa kusini wa jimbo.
Ohio ina eneo la 116,096 km² linalokaliwa na wakazi 11,353,140.
Makala hiyo kuhusu "Ohio" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Ohio kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Majimbo na maeneo ya Marekani |
---|
Majimbo ya Marekani |
Alabama • Alaska • Arizona • Arkansas • California • Colorado • Connecticut • Delaware • Florida • Georgia • Hawaii • Idaho • Illinois • Indiana • Iowa • Kansas • Kentucky • Louisiana • Maine • Maryland • Massachusetts • Michigan • Minnesota • Mississippi • Missouri • Montana • Nebraska • Nevada • New Hampshire • New Jersey • New Mexico • New York • North Carolina • North Dakota • Ohio • Oklahoma • Oregon • Pennsylvania • Rhode Island • South Carolina • South Dakota • Tennessee • Texas • Utah • Vermont • Virginia • Washington • West Virginia • Wisconsin • Wyoming |
Mkoa wa Mji Mkuu |
|
Visiwa vya ng'ambo |
Katika Pasifiki: Samoa ya Marekani • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini • Guam • Katika Karibi: Puerto Rico • Visiwa vya Virgin vya Marekani • Visiwa vidogo sana vya Pasifiki: • Kisiwa cha Howland • Kisiwa cha Jarvis • Atolli ya Johnston • Kingman Reef • Atolli ya Midway • Kisiwa cha Baker • Atolli ya Palmyra • Kisiwa cha Wake • Kisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa |