Austria-Hungaria
Kutoka Wikipedia
Austria-Hungaria ilikuwa milki kubwa katika Ulaya ya Kati na Mashariki kati ya 1867 hadi 1918. Iliendeleza Dola la Austria la awali ikijengwa juu ya ushirikiano wa nchi za Austria na Hungaria zilizotawaliwa na mfalme yeye yule. Nchi hizi mbili zilikuwa na kipaumbele juu ya mataifa mengine ya milki hii kubwa. Mji mkuu ulikuwa Vienna.
Austria-Hungaria iliunganisha nchi na mataifa nyingi. Nchi za leo zilizokuwa ndani ya au sehemu ya Austria-Hungaria ni kama zifuatazo:
- Austria
- Hungaria
- Ucheki
- Slovakia
- Slovenia
- Kroatia
- Bosnia
- sehemu za Poland ya kusini
- sehemu za Romania
- sehemu za Serbia
- sehemu za Italia
Muundo mpya ulianzishwa mwaka 1867 baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe katika Ujerumani 1866 ambako Austria ilishindwa na Prussia.
Hapo Kaisari Franz Joseph I wa Austria aliona haja ya kupata msaada wa Wahungaria waliodai usawa na Wajerumani wa Austria. Kaisari alikubali kupokea taji kama mfalme wa Hungaria akiendelea kutawala kama "Kaisari na Mfalme". Hungaria ilipata bunge lake la pekee.
Milki iliporomoka katika Vita kuu ya kwanza ya dunia. Ilipoonekana ya kwamba Ujerumani na Austria-Hungaria watashindwa sehemu za milki zilianza kutangaza uhuru wao. Hungaria ilijitenga na Austria tar. 31 Oktoba 1918. Kaisari na mfalme wa mwisho Karl I alijiuzulu kama Kaisari na mfalme katika mwezi Novemba 1918.
[hariri] Viungo vya Nje
- "Distribution of Races in Austria–Hungary" from the Historical Atlas by William R. Shepherd, 1911
- The Austro-Hungarian Military
- Austria–Hungary - extensive list of heads of state, ministers, and ambassadors
- Austria-Hungary, Dual Monarchy
- History of Austro-Hungarian currency