Umoja wa Afrika
Kutoka Wikipedia
Umoja wa Afrika (UA) (kiingereza: African Union (AU); kifaransa: Union africaine; Kireno: União Africana ) ni muungano wa nchi 53 za Afrika ulioanzishwa Julai 2002. Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa kiingereza: Organisation of African Union - OAU). Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k. Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuungannisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, ukimwi, n.k.
Yaliyomo |
[hariri] Nchi wanachama
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 53. Ndizo nchi karibu zote za bara la Afrika isipokuwa Moroko iliyoondoka mwaka 1985 kwa sababu ya UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi ya kujitegema wakati Moroko inadai ya kwamba ni eneo la majimbo yake ya kusini. [2]
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.
[hariri] Mikutano mikuu ya UA
- Durban (Afrika Kusini): 9-11 Jul. 2002.
- Maputo (Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
- Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Feb. 2004.
- Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul. 2004.
- Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
- Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Jul. 2005.
- Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.
[hariri] Viongozi
Mwenyekiti wa UA hivi sasa Denis Sassou-Nguesso na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni Alpha Oumar Konaré. Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Getrude Mongella.
[hariri] Viungo vya nje
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |