Syria
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Homat el Diyar "Walinzi wa nchi" |
|||||
Mji mkuu | Dameski |
||||
Mji mkubwa nchini | Dameski | ||||
Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
Serikali
Rais
Waziri mkuu |
Jamhuri Bashar al-Assad Muhammad Naji al-Otari |
||||
Uhuru Ilitangazwa (1) Ilitangazwa (2) Ilitambuliwa |
Septemba 19361 Januari 1 1944 Aprili 17 1946 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
183,885 km² (ya 88) 0.06 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
19,043,000 (ya 55) 103/km² (96) |
||||
Fedha | Lira ya Shamu (SYP ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) |
||||
Intaneti TLD | .sy | ||||
Kodi ya simu | +963 |
||||
1 Mkataba kati ya Ufaransa na Syria ya 1936 haikutambuliwa awali na Ufaransa. |
Syria (Kiar.: سوريا au سورية ) ni nchi ya Mashariki ya Kati au Asia ya Magharibi. Imepakana na Lebanon, Israel, Yordani, Iraq na Uturuki. Kuna pwani la Mediteranea. Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambayo ni kubwa zaidi kuliko Syria ya leo.
Syria ya kisasa imepatikana kama nchi ya kujitawala tangu 1936 kwa ngazi mbalimbali hadi kukamilisha uhuru wake 1946. Kati ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na uhuru wake ule ilikuwa kama nchi lindwa chini ya Ufaransa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa, na kabla ya 1918 ilikuwa sehemu ya Dola la Uturuki. Katika nyakati za kale ilikuwa kitovu cha dola la kwanza la Waarabu na mji mkuu Dameski ilikuwa makao ya makhalifa Wamuawiya.
Syria imetawaliwa na chama cha Baath na rais ni Bashar al-Assad.
Syria kiutawala imegawiwa kwa mikoa au muhafazat 14:
- Al Hasakah
- Al Ladhiqiyah
- Al Qunaytrah
- Ar Raqqah
- As Suwayda
- Dara
- Dayr az Zawr
- Dimashq (Dameski)
- Halab
- Hamah
- Hims
- Idlib
- Rif Dimashq
- Tartus
Wasyria walio wengi ni Waislamu lakini kuna pia Wakristo. Wayahudi wamekuwa wachache sana kutokana na ugomvi kati ya Waarabu na Israel. Waislamu walio wengi ni Wasunni. Kuna pia wafuasi wengi kidogo cha aina ya Washia wanaoitwa "Waalawi".
Lugha ya Kitaifa ni Kiarabu. Kuna pia maeneo penye Wakurdi, Waturuki, Waaramu na wengine.
Syria ilishiriki katika vita za Waarabu dhidi ya ISrael. Sehemu ya Mkoa wa Qunaytrah zimekaliwa na Israel tangu 1967.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hiyo kuhusu "Syria" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Syria kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |