Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Mongolia - Wikipedia

Mongolia

Kutoka Wikipedia

Монгул Улс
Mongol Uls

Jamhuri ya Mongolia
Flag of Mongolia Image:Suld.gif
Bendera Nembo
Wito la taifa: "Dayar Mongol"
Wimbo wa taifa: Bügd Nairamdakh Mongol
Lokeshen ya Mongolia
Mji mkuu Ulaanbaatar
47°55′ N 106°53′ E
Mji mkubwa nchini Ulaanbaatar
Lugha rasmi KiMongolia
Serikali Demokrasia ya kibunge
Nambaryn Enkhbayar
Miyeegombo Enkhbold
Uhuru
Kutangazwa
Kutoka Uchina
Julai 11, 1921
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,564,116 km² (19th)
0.6
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,832,224 (139th)
2,650,952
1.8/km² (227th)
Fedha Tugrug (MNT)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+7)
(UTC+8)
Intaneti TLD .mn
Kodi ya simu +976

Mongolia (Kimongolia: Монгол Улс  mongol uls) ni nchi katika bara la Asia. Imepakana na nchi za Urusi na Uchina. Ni nchi kubwa ya 19 duniani lakini kuna wakazi wachache tu jumla milioni 2.6 hivyo songamano la watu ni kidogo sana. Sehemu za kusini ya Mongolia ya kihistoria ziko ndani ya Jamhuri ya Watu wa China. Hadi 1992 nchi iliitwa Jamhuri ya Watu wa Mongolia.

Yaliyomo

[hariri] Jiografia

Ramani ya Mongolia
Ramani ya Mongolia

Mongolia ni nchi ya mbuga yabisi, majangwa na milima inayofikia kimo cha 4,374 m juu ya UB (Nayramadlin Orgil). Kaskazini ya nchi ina ardhi yenye hali ya sakitu ya kudumu yaani yenye halijoto chini ya 0 C° ndani yake isiyopoa hata wakati wa majira ya joto. Kusini kuna jangwa kubwa la Gobi.

Asilimia 10 pekee za nchi ina misitu hasa mlimani na ardhi inayolimika ni 1 % tu.

[hariri] Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya kibara ina tofauti kubwa. Majira hubadilishana kuwa na joto pia baridi kali. Wastani ya siku ni kati ya −25 °C na +20 °C. Hali halisi wakati wa joto mchana kuna joto kali lakini usiku huwa baridi.

Usimbishaji una tofauti kubwa kati ya kaskazini na kusini ya nchi. Kusini ni yabisi zaidi hadi kushuka kwa 100 mm za mvua pekee kwa mwaka katika jangla la Gobi.

[hariri] Miji

Miji mikubwa ni mji mkuu Ulaanbaatar (Улаанбаатар) (takriban wakazi milioni moja - zaidi ya theluthi ya watu wote wa taifa), halafu Erdenet (wakazi 79,649), Darchan (72,386) na Choibalsan (44,367).

[hariri] Uchumi

Uchumi wa Mongolia hutegemea hasa migodi na ufugaji. Kihistoria Wamongolia walikuwa wafugaji waliohamahama na wanayama wao na kuishi katika hema. Tangu mapinduzi ya 1921 sekta ya migodi na viwanda ilijengwa.

Sekta ya kisasa ya kibiashara iko hasa kwenye mji mkuu.

Hadi leo karibu nusu ya wakazi huishi nje ya miji porini wakifuatana na wanyama wao ambao ni hasa kondoo, mbuzi, ng'ombe, farasi na ngamia. Kilimo kipo mahali pachache kufuatana na tabia yabisi ya nchi. Wakati wa baridi sehemu kubwa ya wafugaji hukaa vijijini walipojenga nyumba.

Migodi ni hasa makaa mawe, shaba, bai na dhahabu.

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Mongolia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Mongolia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


Lugha nyingine


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -