Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Unajimu - Wikipedia

Unajimu

Kutoka Wikipedia

Unajimu ni elimu juu ya nyota jinsi zinavyoonekana kwa macho pamoja na jaribio la kuona uhusiano kati ya nyota na mambo kwenye dunia yetu na katika maisha ya binadamu.

Kuna aina nyingi za unajimu; wengine wanatka kugundua mwendo wa dunia na utabiri wa mambo yajayo, wengine wanaamini ya kwamba wanaweza kutambua tabia ya mwanadamu kutokana na hali ya nyota wakati wa kuzaliwa kwake, wengine wanaona nyota kama alama za miungu.

[hariri] Tofauti ya unajimu na falaki

Unajimu ni tofauti na falaki ingawa zote mbili zilianza na kuendelea pamoja kwa karne nyingi. Tangu mwanzo wa sayansi ya kisasa wataalamu walitambua tabia za nyota kuwa magimba ya angani yenye sifa za kifizikia sio pepo, roho au miungu zinazoweza kutawala dunia au wanadamu. Kwa hiyo njia za unajimu (astrolojia) na falaki (astronomia) zimeachana.

[hariri] Asili ya unajimu

Tangu mwanzo wa historia wanadamu katika sehemu mbalimbali za dunia walitazama nyota wakitambua nyota zinaonekana tofauti na mwendo wa majira. Walitambua pia uhusiano kati ya kuonekana kwa nyota mbalimbali na kutokea kwa mambo yaliyo muhimu kwa maisha ya kibinadamu. Kwa mfano kuonekana kwa nyota fulani (hii inategemea mahali duniani) inaweza kuwa alama ya kwamba mvua ni karibu, au majira ya baridi inaanza.

Watu wa kale walikuwa hodari sana kutazama nyota na kutambua mabadiliko yao katika mwendo wa wakati. Hali hii haieleweki kirahisi na watu wa leo waliozoea nuru ya taa za umeme wakitumia wakati wa usiku kutazama TV au kompyuta. Lakini kwa watu wa kale -jinsi ilivyo hadi leo kwa watu wengi vijijini au porini- nyota na mwezi zilikuwa taa hasa wakati wa usiku.

Uhusuiano ulioonekana kati ya mabadiliko ya nyota na mabadiliko ya majira yalianzisha elimu ya kalenda pamoja na elimu ya unajimu na falaki.

Kwa wazee hawa ilikuwa wazi ya kwamba nyota fulani inatawala majira, hali ya hewa na hivyo maisha ya kibinadamu kwa sababu maisha ya jamii yalitegemea majira na mwendo wa mvua, ukame, baridi au joto. Hapo ni asili ya kuziangalia nyota kama miungu au pepo za enzi. Hasa tabia ya hali ya hewa ya kuchelewa au kuwahi kidogo ilijenga imani ya kwamba kuchelewa kwa mvua ni dalili ya hasira ya mungu yule anayeonekana kama nyota fulani.

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Unajimu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Unajimu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -