Kalenda
Kutoka Wikipedia
Kalenda ni utaratibu wa kupanga wakati. Hupatikana kama orodha ya vipindi vya wakati kama vile siku, juma, mwezi na mwaka. Kalenda mbalimbali zimejua pia vipindi vya miaka kadhaa.
Kalenda inayotumika zaidi leo kimataifa ni kalenda ya Gregori iliyo muhimu kwa uchumi na biashara. Kuna pia nchi zinazotumia hasa kalenda zao za kitaifa au kalenda mbalimbali sambamba.
Hasa maisha ya kidini hupangwa kufuatana na kalenda maalumu. Kihistoria palikuwako na kalenda nyingi.
Yaliyomo |
[hariri] Migawanyo asilia ya wakati
[hariri] Mchana na usiku
Kwa watu wengu duniani mabadiliko wa mchana na usiku ni utaratibu wa kwanza unaogawa wakati. Mchana na usiku pamoja inahesabiwa kama siku moja. Lakini kuna njia tofauti jinsi gani kuanza hesabu hiyo: asubuhi (mwanzo wa mchana) au jioni (mwanzo wa usiku) zilikuwa njia za kawaida za kuhesabu siku mpya. Tangu kupatikana kwa saa zinaonyesha masaa hata gizani saa sita usiki (katikati ya usiku) imeangaliwa kuwa mwanzo wa siku mpya.
[hariri] Awamu za mwezi
Awamu za mwezi huonekana vizuri kwa kila mtu. Kwa sababu hii awamu hizi zilikuwa mbinu unaoeleweka rahisi kupanga siku kwa vipindi. Kipindi kutoka mwezi mpya hadi mwezi mpya ni kipimo kinachopatikana katika kila nchi.
[hariri] Majira kama msingi wa hesabu ya mwaka
Majira au badiliko la vipindi vinavyorudi vya joto na baridi au vya ukame na mvua zilikuwa utaratibu mwingine ulioonekana kwa watu. Ila tu hesabu hii ilitegemea na mazingira na hali ya hewa katika eneo fulani.
Hasa katika nchi ambako majira yanatofautiana vikali na kufuata utaratibu wa kurudia hata mimea na wanyama hufuata mwendo wa majira. Katika mazingira kama hii imewezekana kutofautisha matokeo katika maisha kufuatana na idadi ya vipindi vya baridi au vya joto au vya mvua vilivyopita tangu tokeo fulani.
Mabadiliko ya mimea hutegemea mwendo wa jua na idadi ya mwanga pamoja na joto linalopatikana katika sehemu mbalimbali za dunia. Katika nchi karibu na ikweta tofauti hizi mara nyingi si kali sana na majira hazionekani vizuri isipokuwa majira ya mvua na ukame. Katika nchi hizi kalenda za kale mara nyingi zilitegemea nyota hasa Zuhura (Ng'andu) na mahali angani inapoonekana asubuhi au jioni kwa wakati fulani.
[hariri] Kilimo na mwanzo wa Kalenda
Inaaminika ya kwamba tangu kuanza kilimo watu wameanza pia kushika kumbukumbu ya wakati. Katika nchi nyingi kupanda na kuvuna kunategemea mwendo wa majira yanayorudia. Kazi ya pamoja inahitaji mpangilio na lugha ya pamoja. Hapa ni mwanzo wa kalenda.
[hariri] Tazama pia
Makala hiyo kuhusu "Kalenda" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kalenda kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |