Juma
Kutoka Wikipedia
Juma au wiki ni kipindi cha siku saba. Kila siku ina jina lake. Kuna juma 52 katika mwaka wa kalenda ya Gregori na siku moja au mbili za ziada. Hesabu ya juma inaendelea mfululizo bila kuanza upya wakati wa mwaka mpya. Ufuatano wa juma haulingani na mwgawanyo mwingine wa wakati kwa njia ya miezi au mwaka.
[hariri] Mapokeo ya kiyahudi-kikristo
Asili ya juma ni katika utamaduni wa kale wa Mashariki ya Kati tangu Babiloni. Imeenea kupitia Biblia na kawaida ya Uyahudi na Ukristo.
Ufuatano wa siku katika mapokeo haya huanza na Jumapili. Majina ya siku ni kama yafuatayo:
Siku za Jumamosi na Jumapili mara nyingi huitwa "wikendi" (kiing.: "weekend")
[hariri] Majina ya Siku kwa Kiswahili
Majina ya siku tano kwa Kiswahili ni ya namba zinazoanza kuhesabiwa baada ya siku ya Ijumaa (ambayo ni siku ya sala kuu katika Uislamu):
Ijumaa - Jumamosi - Jumapili - Jumanne - Jumatano.
Alhamisi na Ijumaa ni majina ya Kiarabu. Lugha ya Kiarabu inafuata mapokeo ya Kiyahudi kuhusu majina ya siku.
Hivyo "Alhamisi" ina maana ya "siku ya tano" (baada ya Jumamosi inayoitwa "sabat" kwa Kiarabu sawa kama "shabbat" (=sabato) kwa Kiebrania (lugha ya Kiyahudi).
"Ijumaa" ni matamshi ya Kiswahili ya jina la Kiarabu la "jum'a" inayomaanisha "siku ya mkutano" (= ya kusali pamoja).
Siku za juma (wiki) |
---|
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi |
Makala hiyo kuhusu "Juma" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Juma kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |