Jumatatu
Kutoka Wikipedia
Jumatatu ni siku ya pili katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumapili na Jumanne.
Yaliyomo |
[hariri] Siku ya pili au siku ya kwanza?
Kuna nchi zilizobadilisha hesabu kufuatana na kawaida ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili ambako Jumatatu ni siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda rasmi za serikali hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia.
[hariri] Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "3" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "ya pili".
[hariri] Siku ya mwezi
Katika lugha mbalimbali za Ulaya siku hii ina jina la "mwezi". Lugha hizi kama Kiingereza, Kifaransa au Kijerumani zinaendeleza urithi wa Roma ya Kale na zaidi wa Babiloni ambako kila siku ya wiki ilikuwa chini ya mungu fulani aliyeonekana kama nyota.
[hariri] Jumatatu katika lugha mbalimbali
Lugha | Matamshi | Maana | Maelezo |
---|---|---|---|
Kiebrania | יום שני jom schenai |
siku ya pili | |
Kigiriki | Δευτέρα deutéra |
(siku) ya pili | |
Kiarabu | الاثنين al-ithnayn |
(siku) ya pili | ي |
Kiajemi | دوشنبه do-schanbe |
siku ya pili | |
Kireno | Segunda-feira |
siku ya pili | |
Kilatini | dies lunae | Siku ya mwezi | |
Kiitalia | lunedì | Siku ya mwezi | |
Kihispania | lunes | Siku ya mwezi | |
Kifaransa | lundi | Siku ya mwezi | |
Kijerumani | Montag | Siku ya mwezi | |
Kiingereza | Monday | Siku ya mwezi | |
Kituruki | Pazartesi | baada ya Jumapili (=pazar) |
Siku za juma (wiki) |
---|
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi |