Mfumo wa jua na sayari zake
Kutoka Wikipedia
Mfumo wa jua na sayari zake ni utaratibu wa jua letu na sayari au sayari kibete zinazoizunguka pamoja na miezi yao, asteroidi, meteoridi, kometi na vumbi ya angani yote ikishikwa na mvutano wa jua.
Kwa kawaida huhesabiwa sayari 9 zinazozunguka jua. Lakini miaka ya nyuma magimba makubwa yamegunduliwa angani ambayo bado hayakukubaliwa kama yahesabiwe kuwa sayari au aina ya asteoridi.
Orodha inayofuata bado inahitaji kuangaliwa kwa sababu kuna tofauti kati ya kamusi na vitabu mbalimbali jinsi ya kutaja sayari fulani.
[hariri] Sayari za jua letu
Sayari katika mfumo wa jua ni zifuatazo:
Namba zote zinazotaja sifa mbalimbali za sayari zinaonyesha kipimo kulingana na tabia za dunia yetu kuwa "1"
Jina la sayari | Kipenyo kwenye ikweta kulingana na kipenyo cha dunia = 1 |
Masi | Nusukipenyo ya mzingo wa kuzunguka jua | Muda wa mzingo (miaka) |
Kuinama kwa mzingo wa kuzunguka jua Pembenukta (°) |
Muda wa siku ya sayari (siku) |
Miezi |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Utaridi (Zebaki)* | 0.382 | 0.06 | 0.387 | 0.241 | 7.00 | 58.6 | 0 |
Zuhura (Ng'andu)** | 0.949 | 0.82 | 0.72 | 0.615 | 3.39 | -243 | 0 |
Dunia (Ardhi)*** | 1.00 | 1.00 | 1.00 | 1.00 | 0.00 | 1.00 | 1 |
Meriki (Mars) | 0.53 | 0.11 | 1.52 | 1.88 | 1.85 | 1.03 | 2 |
Mshtarii | 11.2 | 318 | 5.20 | 11.86 | 1.31 | 0.414 | 63 |
Zohari (Zohali) | 9.41 | 95 | 9.54 | 29.46 | 2.48 | 0.426 | 49 |
Uranus | 3.98 | 14.6 | 19.22 | 84.01 | 0.77 | -0.718 | 27 |
Neptun | 3.81 | 17.2 | 30.06 | 164.8 | 1.77 | 0.671 | 13 |
Pluto**** | 0.18 | 0.002 | 39.5 | 248.5 | 17.1 | -6.5 | 3 |
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun |