Neptun
Kutoka Wikipedia
Neptun ni sayari ya nane kutoka jua letu. Ni sayari kubwa ya nne ya mfumo wa jua na mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 17 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake. Hivyo ni nzito zaidi kuliko sayari jirani Uranus lakini ndogo yake.
Ina miezi 13 na bangili nne zisizoonekana rahisi. Mwezi mkubwa huitwa Triton na ukubwa wake hulingana na mwezi wa dunia yetu.
Neptun haionekani kwa macho matupu ni lazima kutumia darubini. Hapo huonekana kama kisahani chenye rangi ya buluu-kijani. Rangi hii imetokana na gesi ya methani inayopatikana kwa wingi katika angahewa yake.
Jina la sayari limetokana na mungu wa Roma ya Kale Neptunus aliyeaminiwa kutawala bahari na mito. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu falaki ya zamani katika tamaduni mbalimbali haikujua sayari hiyo iliyojulikana tangu kupatikana kwa darubini tu.
[hariri] Tazama pia
Makala hiyo kuhusu "Neptun" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Neptun kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun |