Jua
Kutoka Wikipedia
Jua ni nyota ambayo ni karibu yetu zaidi kuliko nyota nyingine. Inazungukwa na sayari tisa. Dunia yetu ni sehemu ya mfumo wa jua na sayari zake.
Kutokana na myeyungano ya kinyukilia ndani yake jua hutoa nishati ambayo ni muhimu kwa maisha ya mimea na viumbe katika dunia. Nishati hii inapatikana kama mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho.
Mada yake ni katika hali ya utegili yaani kama gesi ya joto sana.
Makala hiyo kuhusu "Jua" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Jua kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun |