Orodha ya makabila ya Tanzania
Kutoka Wikipedia
Hii ni orodha ya makabila ya Tanzania.
Kuna matatizo kwenye majina kadhaa katika orodha hii, kwasababu mbalimbali. Orodha hii inatokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za Tanzania, pamoja na tovuti nyingine. Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya. Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kwamba kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vinavyo mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani. Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi kutoka vita katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia au Uhindi.
- Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
- Waakiek
- Waarusha
- Waassa
- Wabarabaig
- Wabembe
- Wabena
- Wabende
- Wabondei
- Wabungu (au Wawungu)
- Waburunge
- Wachagga
- Wadatoga
- Wadhaiso
- Wadigo
- Wadoe
- Wafipa
- Wagogo
- Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
- Wagweno
- Waha
- Wahadzabe (pia wanaitwa Watindiga)
- Wahangaza
- Wahaya
- Wahehe
- Waikizu
- Waikoma
- Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
- Waisanzu
- Wajiji
- Wajita
- Wakabwa
- Wakaguru
- Wakahe
- Wakami
- Wakara (pia wanaitwa Waregi)
- Wakerewe
- Wakimbu
- Wakinga
- Wakisankasa
- Wakisi
- Wakonongo
- Wakuria
- Wakutu
- Wakw'adza
- Wakwavi
- Wakwaya
- Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
- Wakwifa
- Walambya
- Waluguru
- Waluo
- Wamaasai
- Wamachinga
- Wamagoma
- Wamakonde
- Wamakua (au Wamakhuwa)
- Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
- Wamalila
- Wamambwe
- Wamanda
- Wamatengo
- Wamatumbi
- Wamaviha
- Wambugwe
- Wambunga
- Wamosiro
- Wampoto
- Wamwanga
- Wamwera
- Wandali
- Wandamba
- Wandendeule
- Wandengereko
- Wandonde
- Wangasa
- Wangindo
- Wangoni
- Wangulu
- Wangurimi (au Wangoreme)
- Wanilamba (au Wanyiramba)
- Wanindi
- Wanyakyusa
- Wanyambo
- Wanyamwanga
- Wanyamwezi
- Wanyanyembe
- Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
- Wanyiha
- Wapangwa
- Wapare (pia wanaitwa Wasu)
- Wapimbwe
- Wapogolo
- Warangi (au Walangi)
- Warufiji
- Warungi
- Warungu (au Walungu)
- Warungwa
- Warwa
- Wasafwa
- Wasagara
- Wasandawe
- Wasangu
- Wasegeju
- Washambaa
- Washubi
- Wasizaki
- Wasuba
- Wasukuma
- Wasumbwa
- Waswahili
- Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
- Watongwe
- Watumbuka
- Wavidunda
- Wavinza
- Wawanda
- Wawanji
- Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
- Wayao
- Wazanaki
- Wazaramo
- Wazigula
- Wazinza
- Wazyoba