Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Wachagga - Wikipedia

Wachagga

Kutoka Wikipedia

Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.

Wachagga ni kabila tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.

Yaliyomo

[hariri] Vikundi vya Wachagga

Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine na ndiyo sababu lugha yao, Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea, Rombo magharibi ya Kilimanjaro mpaka unapofika Siha, Machame magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika makundi ya Kichagga cha Rombo, Marangu, Old Moshi,Kibosho, na Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vonjo, Wa-Uru, na Wa-siha. Baadhi ya wachagga walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wachagga wa Machame ingawa lafudhi zao zinatofautiana desturi na mila zao ziko karibu sana.

[hariri] Historia ya elimu kati ya Wachagga

Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kati ya kabila lenye watu wengi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro kuwa unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania.

Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.

Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu.


[hariri] Kilimo na chakula

Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe,viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.

[hariri] Ndizi za Wachagga

Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama mtori machalari, kiburu na kadhalika.

Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.

Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.

[hariri] Wachagga na muhogo

Inasemekana kuwa "mchagga halisi, hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mambu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za muhogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea tabia hii wana njia za kuondoa sumu kwa mfano kwa kuiacha mizizi katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea.

[hariri] Majina ya Kichagga

Familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Moshi, Lema, Urassa, Nkya, Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Tesha, Mariki, Tarimo, Laswai, Ndosi, Mallya, Kimambo, Sawe, Usiri,Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Rite, Makule, Kimambo, Minja, Mrema, Mramba, Njau, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo,Mafole, Kituo, Mroso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro,Matowo, Towo, Meena, Mkony, Temba na kadhalika.

Pia inasemekana kuwa, Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Kikristo, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchaggani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao

[hariri] Maoni juu ya Wachagga

Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. Wanawake wa kichagga hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shunguli za kiiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chaula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.

[hariri] Viungo vya nje

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Wachagga" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Wachagga kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -