Kabohidrati
Kutoka Wikipedia
Kabohidrati ni kampaundi ya kikemia kinachojengwa kwa oksijeni, hidrojeni na kaboni. Katika kemia huitwa kwa jumla kwa jina "sukari" hata kama sukari kwa lugha ya kawaida ni sehemu ya kabohidrati tu.
Kabohidrati ni kati ya molekuli muhimu zinazojenga viumbehai na mimea duniani. Kazi zao ni nyingi kwwa mfano kuhifadhi na kubeba nishati (wanga) ndani ya mwili wa wanyama na mimea au kujenga mwili kwa umbo la selulosi au chitini cha wadudu.
Umbo la kimsingi wa kabohidrati ni monosakaridi (Cn(H2O)n) zinazoungana kuwa aina nyingine za kabohidrati.
Aina za kabohidrati ni kwa mfano:
- monosakaridi (glukosi, fruktosi)
- disakaridi (sukrosi yaani sukari ya kawaida)
- polisakaridi (wanga, selulosi)
[hariri] Chakula
Kabohidrati ni chanzo cha nishati katika chakula cha watu wengi. Takriban asilimia 40 - 75 za mahitaji ya nishati ya watu hutokeana na kabohidrati. Vyakula vyenye kabohidrati nyingi ni vile vyenye wanga hasa nafaka na vyote vilivyotengenezwa kwa kutumia nafaka kama vile ugali, mkate, pasta, wali pamoja na mazao kama viazi na ndizi.
Katika utamaduni chache watu hula kabohidrati kidogo na karibu chakula chote ni protini ya kinyama kama vile Eskimo au Massai wanaokula hasa protini lakini mwili unaweza kubadilisha protini kuwa kabohidrati isipokuwa lishe yake inapungua.