Hidrojeni
Kutoka Wikipedia
Hidrojeni (Hydrogenium) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Hidrojeni (Hydrogenium) |
Alama | H |
Namba atomia | 1 |
Mfululizo safu | Simetali |
Uzani atomia | 1.00794 |
Valensi | 1 |
Densiti | 2700 kg/m3 |
Kiwango cha kuyeyuka | 14.02 K (−259.12°C) |
Kiwango cha kuchemka | 20.27 K (−252,88°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.88 |
Hidrojeni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 1 na uzani wa atomi 1.00794. Alama yake ni H. Ni atomi nyepesi kati ya elementi zote hivyo ina nafasi ya kwanza katika mfumo radidia
Hidrojeni ni elementi inayopatikana kwa wingi kabisa ulimwenguni lakini si duniani. Iko ndani ya maji na katika molekuli zote za mada hai.
[hariri] Muundo wa atomi
Atomi za H zina elektroni moja tu inayozunguka kiini cha atomi. Hidrojeni ya kawaida ina protoni moja tu. Hii ni zaidi ya asilimia 98 ya isotopi zote za hidrojeni. Kuna pia isotopi yenye nyutroni moja au mbili katika kiini lakini zinatokea mara chache tu.
[hariri] Kupatikana kwake ulimwenguni
Duniani kwa kawaida hakuna hidrojeni ya atomi moja moja hutokea kama gesi yenye molekuli za H2.
Masi ya jua letu ni hasa hidrojeni lakini pia sehemu kubwa ya masi za sayari kubwa yaani Mshtarii, Zohali, Uranus na Neptun. Kwa jumla asilimia 93 za atomi zote na asilimia ya masi katika mfumo wa jua letu ni H.