Kaboni
Kutoka Wikipedia
Kaboni ni elementi yenye namba atomia 6 na uzani atomia 12 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni C. Inapatikana pekee yake kwa umbo mbalimbali kama vile makaa au almasi lakini mara nyingi katika michanganyiko ya kikemia.
Kati ya tabia za kaboni ni uwezo wake wa kujiunga na elementi nyingi hivyo kuunda molekuli kubwa.
Kaboni ni elementi muhimu zaidi pamoja na oksijeni katika vyumbehai vyote pamoja na mimea. Iko katika idadi kubwa ya kampaundi ogania.
Kiteknolojia kaboni ni muhimu kwa sababu ni kimsingi wa aloi zote za chumapua na hivyo teknolojia ya kisasa. Kwa upande mwingine kaboni iko pia katika aina zote za plastiki.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Kaboni" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kaboni kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |