Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Divai - Wikipedia

Divai

Kutoka Wikipedia

Divai nyekundu ny nyeupe

Divai (pia: mvinyo) kinywaji cha pombe kinachotengenezwa kwa maji ya zabibu. Inawezekana kutumia pia maji ya matunda mengine na kupata kinywaji cha kufanana ingawa watu wengine hawapendi kuiita "divai".

Yaliyomo

[hariri] Zabibu na divai

Kimsingi maji ya zabibu huwa divai kwa kuchachuka kwa sukari ndani yake. Zabibu hupondwa zikiachwa katika chombo kikubwa kwa kuchachua. Maji ya mizabibu huwa na sukari nyingi pamoja na asidi ndani yake inayohitajika kwa ladha inayolengwa. Divai safi haitakiwa kupewa nyongeza yoyote. Nyongeza zinazotokea ni hasa sukari kama kiwango chake ndani ya zabibu hakitoshi. Kazi ya kuchachua inaendelea kwa kawaida kutokana na hamira asilia zinazokaa kwenye maganda; lakini inawezekana pia kuongeza hamira za pekee.

[hariri] Aina za divai

Aina mbili zinazotengenezwa hasa ni divai nyekundu na divai nyeupe.

Divai nyeupe hupatikana kama maji ya zabibu pekee huchachua. Divai nyekundu inapatikana kama tunda lote yaani maji pamoja na maganda huchachua.

Kuna aina za divai za kuchemka yaani zinatoa viputo vya gesi vidogo vidogo. Maarufu kati ya divai hizi ni shempeni kutoka mkoa wa Champagne katika Ufaransa.

[hariri] Divai katika historia

Divai imejulikana tangu miaka mingi; kuna dalili za kiakolojia ya kwamba imepatikana katika sehemu za Uajemi na Kaukazi tangu 5000 KK. Imekuwa sehemu ya utamaduni ya nchi nyingi hasa katika mashariki ya kati na nchi za Mediteranea. Waroma wa Kale waliipeleka katika sehemu zote za dola lao. Lakini upatikanaji umetegemea na hali ya hewa; divai inahitaji kiwango chake cha jua na mvua kwa hiyo kwenye tabianchi za kaskazini ya Ulaya divai haistawi.

[hariri] Divai katika dini

Iliingia pia katika dini za Misri, Babeli na Ugiriki ya Kale. Osiris (Misri), Dionisi (Ugiriki) na Gilgamesh (Bebali) walikuwa miungu iliyohusika divai ama kwa kuileta kwa wanadamu au kwa kulinda kilimo chake.

Katika Biblia Nuhu anatajwa kama mnywaji wa kwanza wa divai. Katika kitabu cha Zaburi divai ni ishara ya furaha, kwa mithali ni dawa la mwenye huzuni lakini kuna pia maonyo dhidi ya hatari za ulevi.

Yoshua Bin Sira: 31:27-29 ”Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji ya uzima, ukinywa kwa kiasi. Je, anao uzima gani mtu asiye na mvinyo? Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu. Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho, ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha. Lakini kunywa mno ni uchungu wa roho, na fedheha, na ugomvi.”

Katika Agano Jipya Yesu anatumia divai na mzabibu kama ishara za uzima wa milele na pia kwa umoja wa watakatifu. Jinsi ilivyo katika Uyahudi kwenye ibada ya jioni ya Sabato divai ni sehemu za ibada ya Ekaristia au chakula cha Bwana.

Uislamu ni dini ambamo wafuasi wengi hupinga divai pamoja na vinywaji vya kileo. Qurani yenyewe ina matamko mbalimbali juu ya divai. Mizabibu ni sehemu ya uumbaji wa Allah (sura 16, 10-11), kwenye Paradiso waumini watakuwa na maji, maziwa, divai na asali tele (sura 47,15). Sura 2,119 inaona pande mbili kwenye divai: "Wanakuuliza juu ya divai (Kar. khamar)[1] na kamari. Sema: Katika hivyo mna madhara makuu na manufaa kwa watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake." Katika sura 5, 90-91 divai hutajwa kama uchafu na kazi ya sheitani.

Aya hizi zinachukuliwa na wataalamu wengi kama kupiga marufuku divai na kileo kwa jumla; wataalamu wachache huona ya kwamba Qurani haitumii neno "haramu" kwa hiyo wanataka kupiga marufuku si divai yenyewe lakini kiasi kile kinacholeta ulevi. Hoja la kupiga ulevi wote marufuku limekuwa hoja kuu kati ya Waislamu inaonekana pia katika hadith kadhaa za mtume Mohammed.

lita 1-7 lita 7-15 lita 15-30 lita zaidi ya 30
lita 1-7
lita 7-15
lita 15-30
lita zaidi ya 30

[hariri] Nchi zinazovuna divai kwa wingi

Zabibu zinazofaa kwa divai zinastawi vizuri duniani kati ya latitudo ya 30 na 50 upanda wa kusini na kaskazini ya ikweta.

Mavuno ya zabibu katika nchi muhimu 2006[2]
Nafasi Nchi
Zao
(tani)
1 Ufaransa 5,349,333
2 Italia 4,711,665
3 Hispania 3,643,666
4 Marekani 2,232,000
5 Argentina 1,539,600
6 Australia 1,410,483
7 China 1,400,000
8 Afrika Kusini 1,012,980
9 Chile 977,087
10 Ujerumani 891,600


[hariri] Viungo vya Nje


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -