Beijing
Kutoka Wikipedia
Beijing (pia: Peking) ni mji mkuu wa China. Iko katika kaskazini-mashariki ya nchi. Rundiko la jiji lina wakazi wapitao milioni 15. Tangu karne sita imekuwa kitovu cha utawala wa China. Jina lenyewe lamaanisha "Mji Mkuu wa Kaskazini" kwa sababu China iliwahi kuwa na vitovu mbalimbali hasa Nanjing (mji mkuu wa kusini).
Kiutawala jiji la Beijing pamoja na maeneo ya jirani hutawaliwa kama mkoa wa nchi mwenye eneo la 16,800 km².
Kutokana na historia ndefu kuna majengo mengi mazuri yanayohifadhiwa hata kama mitaa mingine inabadilika haraka. Sehemu ianyohifadhiwa ni pamoja na Uwanja wa Tianamen, Mji Haramu pamoja na nyumba za makaisari wa China na mahekalu mbalimbali.
Leo hii Beijing ni mji mkubwa wa pili katika China baada ya Shanghai. Katika historia iliwahi kuwa mji mkubwa duniani kati ya karne ya 13 hadi 18.
Mwaka 2008 Beijing itakuwa mwenyewi wa michezo ya Olimpiki.
Makala hiyo kuhusu "Beijing" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Beijing kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |