Mtakatifu Paulo
Kutoka Wikipedia

Mtakatifu Paulo (BK 3-62) alizaliwa katika familia ya kiyahudi. Nyumbani kwao ni mji wa Tarsus (kwa sasa mji huo uko katika nchi ya Uturuki). Jina la kwanza nalijulikana kama Sauli. Angali kijana alipinga Ukristo kwa kuwakamata, kuwatesa na hata kuwaua Wakristo. Wakati huo alikutana na Yesu Kristo kwa njia ya maono akiwa njiani kwenda Damaski (hadithi inasimuliwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16). Alifanya safari tatu muhimu za kitume. Paulo alikamatwa na wapinzani wake Wayahudi mjini Jerusalemu na kupelekwa Roma. Alizungumzia kifo chake (kufuatana na Matendo ya Mitume 20:24) na kuuawa Roma kati ya BK 62. Aliandika barua nyingi kwa makanisa ya Efeso, Galatia, Roma, Korinto, na kwa viongozi Wakristo kama Timotheo n.k.