Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Mkoa wa Tanga - Wikipedia

Mkoa wa Tanga

Kutoka Wikipedia

Mkoa wa Tanga katika Tanzania
Mkoa wa Tanga katika Tanzania
Wilaya za Mkoa wa Tanga
Wilaya za Mkoa wa Tanga

Mkoa wa Tanga ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Makao makuu yako Tanga mjini.

Yaliyomo

[hariri] Eneo la mkoa

Mkoa una eneo la 27,348 km² na uko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji.

Kuna wilaya saba ambazo ni Lushoto, Korogwe, Muheza, Handeni, Kilindi, Pangani na Tanga Mjini. Eneo linalofaa kwa kilimo ni 17,000 km². Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake.

Wilaya au manisipaa Eneo km² Wakazi (2002) Tarafa Kata Kijiji
1 Tanga mjini 536 243,580 4 21 23
2 Muheza 4,922 279,423 6 27 140
3 Korogwe 3,756 261,004 4 20 132
4 Lushoto 3,500 419,970 8 32 137
5 Handeni 13,209 393,931 13 23 102
6 Pangani 1,425 44,107 4 13 23
Jumla 1,642,015 27,348 37 136 557
(Wilaya ya Handeni imegawanywa kuwa wilaya mbili za Handeni na Kilindi)


[hariri] Wakazi

Makabila makubwa mkoani Tanga ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo. Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milimani ya Usambara, Muheza, Korogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.

Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga penyewe na sehemu za Muheza.

Msongamano wa wakazi ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto penye ardhi yenye rutuba nzuri.

[hariri] Hali ya hewa

Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto ikiwa pakavu zaidi. Milima ya Usambara hapana joto sana. Miezi ya Desemba - Machi halijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.

Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi takriban milimita 1,100 hadi 1,400 mm ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka.

[hariri] Uchumi

Wakazi wengi hutegemea kilimo cha riziki pamoja na ufugaji na uvuvi. Mazao ya chakula hasa ni mahindi, muhogo, ndizi, maharagwe na mpunga.

  • Mazao ya biashara ni katani, pamba, kahawa, chai, nazi, tumbaku na korosho.
  • Mifugo ni ngombe, mbuzi na kondoo pamoja na kuku.
  • Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba haya yalikuwa ya walowezi, yalitaifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani inategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ilirudi nyuma tangu miaka ya 1960.

Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu zote zimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizai mali kulingana na uwezo wao. Kilichobaki ni hasa kiwanda cha saruji Tanga.

Utalii umeanza kupanua kidogo hasa katika eneo la Pangani na Mapango ya Amboni.

[hariri] Viungo vya nje


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -