Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Mkoa wa Kigoma - Wikipedia

Mkoa wa Kigoma

Kutoka Wikipedia

Mkoa wa Kigoma katika Tanzania
Mkoa wa Kigoma katika Tanzania

Kigoma iko kati ya mikoa 26 za Tanzania. Imepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa la Tanganyika penye mpaka na Kongo.

Kuna wilaya nne ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Kigoma Mjini (144,852), Kigoma Vijijini (490,816), Kibondo (414,764), Kasulu (628,677). Jumla ya wakazi ni 1,679,109 (sensa 2002). Makao makuu ndipo Kigoma mjini.

Yaliyomo

[hariri] Eneo la Mkoa

Mkoa una eneo la 45,066 km² (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa 8,029 km² ndizo maji hasa Ziwa la Tanganyika na 37,037 km² ndizo nchi kavu.

Wilaya au manisipaa Eneo km² nchi kavu km²  % za mkoa wote Tarafa Kata Kijiji
1 Kigoma mjini na vijijini 19,685 11,655 31 7 31 71
2 Kibondo 16,058 16,058 44 4 20 66
3 Kasulu 9,324 9,324 25 7 30 83
Jumla 45,066 37,037 100 18 81 220

,

Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu.

Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye UB wa 800m karibu na Ziwa la Tanganyika na kupanda hadi 1,750 m.

Mito ya kudumu ndiyo Malagarasi, Luiche na Ruchugi.


[hariri] Wakazi

Kabila kubwa ndilo Waha. Kuna pia Wanyamwezi, Wasukuma, Wafipa na watu wenye asili ya Kongo, Rwanda na Burundi.na pia wapo wa [manyema ambao ndio wa starabu kuliko kabila lolote kati ya makabila ambayo yana ishi mkoani hapo

Idadi au msongamano wa watu katika maeneo ya mkoa huu imetegemea sana kupatikana kwa inzi za aina ya ndorobo. Penye ndorobo wengi watu ni wachache.

[hariri] Uchumi na mawasiliano

Mkoa wa Kigoma haukuona bado maendeleo yanayolingana na mazingira yake. Hali ya barabara na mawasiliano mengine ni mbaya. Umbali hadi Daressalaam ni 1316 km, hadi Mwanza 830 Km, hadi Arusha 1204 Km. Lakini hakuna barabara ya lami hata barabara za kokoto ni sehemu ndogo to.

Usafiri muhimu ni reli ya kati kutoka Kigoma kwenda Daressalaam kupitia Tabora na Dodoma. Isipokuwa reli hii imeshazeeka ilhali imejengwa zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Treni zake huchelewachelewa zinachukua muda mrefu. Wakati wa mvua inatokea ya kwamba mawasiliano yanavurugika.

Uwanja wa ndege wa Kigoma inashughulika ndege ndogo aina ya Fokker.

Mnamo 85% ya wakazi wote hutegema kilimo, walio wengi kilimo cha kujitegemea tu.

Kuongezeka kwa wakimbizi kutoka nchi jirani na kukua kwa makambi kulikuwa tatizo kubwa.


[hariri] Hifadhi za wanyama na za kihistoria

Kuna maeneo mawili penye sokwe: ndipo Hifadhi ya Taifa ya Gombe (alikofanya utafiti wake mwanabiolojia Jane Goddall) na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.

Mji wa Ujiji ulioko karibu na Kigoma mjini ndio mji wa kale zaidi katika Tanzania ya Magharibi penye makumbusho wa Dr. Livingstone.

[hariri] Viungo vya Nje


 
Mikoa ya Tanzania
Bandera Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -